NAIBU KATIBU MKUU AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu amesema Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wanapaswa kuendana na mabadiliko ya Teknolojia wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Desemba 01 hadi Desemba 03 mwaka 2021.


Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Dkt. Kazungu amesema Wahasibu na Wakaguzi wa fedha ni watu muhimu katika maendeleo hususani uchumi wa viwanda hivyo wanapaswa kujipima na kuona umuhimu wao katika jamii.


"Wahasibu ndiyo wanaofanya uchambuzi wa mambo ya fedha na kuandaa ripoti za hesabu za fedha na uhakika ambazo zinasaidia katika ukusanyaji wa kodi, kuimarisha uchumi na kuvutia uwekezaji," Amesema Kazungu.


Amesema katika wimbi hili la Mapinduzi ya Viwanda ambayo yanahusisha teknolojia hivyo wanapaswa wajipange vizuri Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ili kuendana na mapinduzi hayo, pia amesema suala la maadili ni suala nyeti kwenye utumishi wa umma hususani kwanye taaluma ya Uhasibu kwasababu Wahasibu ndio wanaotunza hesabu hivyo inabidi wasimamie maadili ili kuepuka hati chafu kwenye Taasisi mbalimbali.


Pia amesema Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wanayo nafasi kubwa kufanikisha safari ya uchumi wa viwanda, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kujiona kuwa ana deni kwa Taifa ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu amesema katika mageuzi ya teknolojia na mapinduzi ya kiuchumi duniani inahitaji Wahasibu ambao wanaweza kwenda na teknolojia pamoja na kuwa uwezo wa kuchakata takwimu mbalimbali ambazo zinaongeza tija na thamani katika maeneo mbalimbali ya kazi.


Amesisitiza kuwa elimu waliyonayo Wahasibu haitoshi kwa sasa hivyo wanapaswa kuelewa vizuri mabadiliko ya Teknolojia hasa kwenye ukuaji wa uchumi wa Taifa bado wanahitajika Wahasibu wengi kwani wahasibu waliopo hawatoshi hivyo zitolewe elimu kwenye vyuo pamoja na shule ili kuleta hamasa kwa wanafunzi kupenda fani hiyo.


Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa mwenyekiti wa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwani nafasi hiyo ni nzito hivyo atasimama vizuri ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea kama Bodi.


Akizugumza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema kwamba Bodi hiyo ina majukumu makubwa matano ambayo ni kusajili Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu. Kusimamia taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi, kusimamia mafunzo na kutoa vyeti vya kitaaluma, kutoa muongo wa utayarishaji wa hesabu na ukaguzi wa hesabu.


Amesema Bodi hiyo inazingatia viwango vya kimataifa vya uandishi wa vitabu na ukaguzi. Hivyo Tanzania kupitia NBAA inaendelea kusimamia matumizi ya viwango vya kimataifa vya utayarishaji na ukaguzi wa taarifa za fedha katika Serikali Kuu na idara zake, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kwa kushirikiana na Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wa hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu akizungumza kuhusu Serikali inavyothamini mchango wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu hivyo itasimamia taaluma hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ulioandaliwa na Bodi ya NBAA uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu alimwakilisha Waziri Wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu akizungumza kuhusu namna alivyojipanga kama Mwenyekiti mpya pamoja na kusimamia ipasavyo Bodi hiyo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ili kuendana na Kauli ya Rais Samia ya Kazi iendelee wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza kuhusu namna Bodi hiyo inavyofanya kazi pamoja na mafanikio waliyoyapata ndani ya muda mchache wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa, wanyakazi wa Bodi ya NBAA, Wahasibu na Wakaguzi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu aliyemwakilisha Waziri Wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Wahasibu na Wakaguzi uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika Hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika leo Desemba 01, 2021 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib Kazungu akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadhamini, Viongozi mbalimbali wa Serikali na Bodi hiyo pamoja na Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2021 wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments