MCHUNGAJI ALIYEBAKA MWANAKWAYA AJITETEA


KASISI wa Kanisa moja huko Abeokuta katika Jimbo la Ogun nchini Nigeria, Peter Taiwo amejitetea kuwa hakumbaka mwanakwaya mwenye umri wa miaka 16 katika kanisa lake na kusema wawili hao ‘walipendana.’

Akijitetea polisi baada ya mamlaka kufunga shughuli za kanisa hilo na pia kumshikilia mkewe kwa uhalifu huo, Taiwo alisisitiza yeye na msichana huyo wa miaka 16 walipendana.

“Nilimuomba aachane na mpenzi wake na kwamba nitatoa chochote ambacho angehitaji,” aliliambia Jeshi la Polisi.

Ukaribu na msichana huyo ulianza baada ya kupata jeraha la mguu. Kulingana taarifa yake, Kasisi huyo alimsaidia msichana huyo na wazazi wake kwa kumlipia gharama za matibabu na pia kumwombea.

Jambo hilo, anadai liliwaleta karibu na kwamba msichana alikuwa huru kuingia katika chumba chake cha kulala.

Taiwo alisema: “Anakuja chumbani kwangu, tunazungumza, tunazungumza pamoja. Siku moja alipokuja asubuhi kwa ajili ya matibabu ya mguu wake, nilimuita ndani ili niuone mguu wake, sikujua roho iliyonijia nikiwa naukagua mguu wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments