Breaking

Post Top Ad

Saturday, December 11, 2021

ASKARI POLISI AMUUA KWA KUMPIGA RISASI ASKARI MWENZAKE


Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi.

amanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi, amesema jeshi hilo limemfukuza kazi askari namba H.2324 PC Joseph kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi askari mwenzake Onesmo Joseph, baada ya marehemu kuchelewa kurejesha pikipiki ya mtuhumiwa aliyokuwa ameazima na ndipo wakaanza kuzozana.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi, amesema kwamba tukio la kumfyatulia mwenzake risasi lilitokea wakati wote wawili wakiwa kwenye lindo la benki ya CRDB tawi la Ruangwa mkoani humo.

"Taarifa za awali zinaonesha kwamba marehemu alimuazima pikipiki askari mtuhumiwa, sasa alipochelewa kumrudishia kwenye ule muda waliokubaliana ugomvi kati yao uliendelea ukawafikisha hapo walipofikia," amesema Kamanda Kitinkwi.

Chanzo - EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages