Breaking

Post Top Ad

Wednesday, December 8, 2021

MWENDESHA BODABODA AMUUA MCHUMBA WAKE, NAYE AJIUA


Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Mwango Nzioka mwenye umri wa miaka 30 aliyekuwa akifanya kazi ya kuendesha bodaboda, amemuua mpenzi wake, Mercy Gichuhi kisha naye kujiua, tukio lililotokea katika eneo la Mitaboni, Kaunti ya Machakos nchini Kenya.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo liligundulika na mmoja kati ya wasichana waliokuwa wakifanya kazi ya kuuza baa na marehemu Mercy, ambao walifika nyumbani hapo kuchukua funguo baada ya kuona mwenzao hajafika kazini asubuhi kama kawaida, huku akiwa na funguo za ofisi.


Kwa mujibu wa baba wa marehemu ambaye anafanya kazi ya ulinzi, Peter Kaloki mara ya mwisho kumuona mwanaye na mchumba wake huyo ambaye alikuwa akiishi naye, ilikuwa ni Jumatatu usiku ambapo walirejea kutoka kwenye matembezi ya jioni huku kukiwa hakuna dalili zozote za ugomvi kati yao.


Anazidi kueleza kwamba, kesho yake asubuhi baada ya kurejea kazini, alipata kifungua kinywa kisha kupumzika lakini ilipofika majira ya saa saba za mchana, aliamshwa na mkewe ambaye alimpa taarifa za kushtua kwamba mwanaye huyo amefariki.


Kaloki anaeleza kwamba aliongozana na mkewe mpaka kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mwanaye huyo, ambayo ipo eneo mita chache kutoka kwenye nyumba anayoishi ambapo baada ya kuingia ndani, alimkuta mwanaye akiwa ananing’ia kwenye dari akiwa amejinyonga, huku mchumba wake akiwa amelala kitandani, akionesha kukabwa shingo yake na nguo mpaka kupoteza fahamu.


Kaloki anaeleza kwamba baada ya kukuta hali hiyo, walipiga simu polisi ambao walikuja saa kadhaa baadaye na kuichukua miili yote na kuipeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Machakos huku uchunguzi ukiendelea kuhusu tukio hilo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages