ANUSURIKA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUMSHAMBULIA MKE NA WATOTO AKIHISI ANATAKA KUACHWA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, December 21, 2021

ANUSURIKA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUMSHAMBULIA MKE NA WATOTO AKIHISI ANATAKA KUACHWA


JESHI la Polisi katika eneo la Kisii nchini Kenya wanamshikilia Daniel Asiago kwa kumshambulia na kumjeruhi kwa kumkatakata Mke wake na Watoto wawili katika Kijiji cha Gesoni kwa kile kinachodaiwa chanzo ni kuhisi mke huyo anataka kumuacha.

Polisi wanasema baada ya tukio hilo Raia wenye hasira kali waliamua kuichoma nyumba ya mwanaume huyo moto na wakawa wanataka kumuua lakini akafanikiwa kukimbia kwa bodaboda na kujisalimisha kituo cha Polisi Nyatieko ambapo sasa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani leo Jumatatu, Desemba 20, 2021.

Majirani wanasema hiyo sio mara ya kwanza kwa wawili hao kugombana na inadaiwa Mwanaume hawapendi Watoto hao kwakuwa Mke alikuja nao tu kwenye ndoa kutoka kwa Baba mwingine miezi minne iliyopita, Mke na Watoto wamelazwa Hospitali wakiendelea kutibiwa.
Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages