SEKTA ZA UWEKEZAJI KUBORESHA HUDUMA ILI KUONGEZA MAPATO


Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji Geoffrey Mwambe (aliyesimama) akieleza namna ya kupunguza vikwazo wanavyokumbana navyo wawekezaji nchini ili kuongeza mapato yatakaenda kusaidia ujenzi wa miundombunu na kuboresha huduma. 

Wataalamu wa mifumo na wadau mbalimbali katika sekta ya uwekezaji wakiwa katika kikao cha mazmio yenye lengo la kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wawekezaji ili taasisi zinashoghulikia wawekezaji kuweka mfumo mzuri hivyo kupunguza msululu upatikanaji wa leseni kwa wawekezaji hao. 

Baadhi ya wajumbe wa sekta zilizo chini ya wizara ya uwekezaji ikiwemo kituo cha huduma za uwekezaji nchini (TIC) wakifuatilia kwa makini mjadala uliokuwa ukiendelea juu ya kupunguza vikwazo wanavyokumbana navyo wawekezaji nchini ili kuongeza mapato yatakaenda kusaidia ujenzi wa miundombunu na kuboresha huduma. 

****************** 

Sekta zilizo chini ya Wizara ya Uwekezaji ikiwemo kituo cha Huduma za uwekezaji Nchini (TIC) imedhamiria kupunguza vikwazo wanavyokumbana navyo wawekezaji nchini ili kuongeza mapato yatakaenda kusaidia ujenzi wa miundombunu na kuboresha huduma kwa jamii ikiwa ni kuunga mkono dhamira Rais wa jamhuri a muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anawaondolea kero wananchi wake 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Geoffrey Mwambe Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa mifumo na wadau mbalimbali katika sekta ya uwekezaji chenye lengo la kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wawekezaji hao, amesema Mamlaka zote na Taasisi zinashoghulikia wawekezaji kuweka mfumo mzuri ili kupunguza msululu upatikanaji wa leseni kwa wawekezaji hao. 

Naye Mkurugenzi mtandaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Dkt Maduhu Kazi akaeleza namna mfumo huo utaweza kurahisisha kutoa huduma bora kwa wawekezaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments