Picha : WAJUMBE WA BODI MENEJIMENTI NA WAFANYAKAZI WA TUZ WAZURU TCRA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliozuru ofisi za Mamlaka kwa lengo la kujifunza namna TCRA inavyosimamia mawasiliano. Katika ziara hiyo TCRA na TUZ wameashiria nia ya kuhuisha baadhi ya vipengele vya mashirikiano baina ya taasisi hizo mbili kwa lengo la kuboresha huduma wanazosimamia. Picha na: TCRA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliozuru ofisi za Mamlaka kwa lengo la kujifunza namna TCRA inavyosimamia mawasiliano. Katika ziara hiyo wamepata ufafanuzi juu ya mfumo wa ugawaji na usimamizi wa masafa, utangazaji na utoaji wa leseni za mawasiliano. Picha na: TCRA

Mkuu wa Kitengo cha Leseni katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akifafanua ukuaji wa teknolojia ya utangazaji katika kipindi cha Miaka Sitini ya Uhuru wa Tanzania katika Makumbusho ya Mawasiliano mbele ya wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) walifanya ziara ya mafunzo kujifunza namna TCRA inavyosimamia sekta ya mawasiliano Tanzania. Picha na: TCRA Mkuu wa Kitengo cha Leseni katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliofanya ziara ya mafunzo ofisi za TCRA kupata uelewa wa namna Mamlaka hiyo inavyosimamia sekta ya mawasiliano Tanzania. Picha na: TCRA.

Mhandisi Mwandamizi wa Masafa katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Victor Kweka akitoa wasilisho mbele ya Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliozuru ofisi za TCRA Makao Makuu kwa ziara ya mafunzo. TUZ imebainisha kuboresha zaidi utoaji huduma za mawasiliano Zanzibar baada ya ziara hiyo ikiwemo maandalizi ya kupokea mabadiliko ya TEHAMA katika kuboresha sekta ya mawasiliano Zanzibar. Picha na: TCRA

Mhifadhi wa Makumbusho ya Mawasiliano inayosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bi. Jasmine Kiyungi akifafanua ukuaji wa sekta ya mawasiliano mbele ya Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar waliozuru TCRA kujifunza namna mawasiliano yanavyosimamiwa. TUZ imeweka bayana dhamira yake kuboresha zaidi huduma zake mara baada ya ziara hiyo ya mafunzo. Picha na: TCRA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments