MAHAFALI YA 14 YA CHUO KISHIRIKI CHA ELIMU DAR ES SALAAM (DUCE) YAFANA

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwatunuku wahitimu wakati wa mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akifurahi jambo wakati wa mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza wakati wa mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam. Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.Stephen Maluka akizungumza wakati wa mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Wahitimu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam wakifuatilia mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam. Wahitimu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam wakifurahi wakati wa mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO NA UDSM)

******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

UVIKO-19 imeendelea kuathiri shughuli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwani makongamano, tafiti na ubunifu na shughuli nyingine zinazohusisha mikusanyiko ya watu zilifanyika kwa tahadhari kubwa au kwa njia za mitandao pale ilipobidi.

Ameyasema hayo leo Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.William Anangisye kwenye Mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

Amesema UVIKO-19 umeathiri kwa kiasi kikubwa mchakato wa ununuzi wa vifaa vya ujifunzaji na ufundishaji na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo.

Pamoja na hayo amesema wanafunzi wapatao 1,565 watahitimu na kutunukiwa digrii na Stashahada mbalimbali.Wahitimu hao ni kutoka katika kitivo cha Sayansi za Jamii, Kitivo cha Elimu na Kitivo cha Sayansi.

Aidha Prof.Anangisye amesema katika mwaka wa masomo 2020/2021, Chuo kimeanzisha ushirikiano na Taasisi 5 za Kimataifa katika nyanja mbalimbali hasa tafiti, utoaji wa mafunzo na ubadilishanaji wa ujuzi na maarifa.

"Wahitimu wanafahamu kuwa ingawa wao ndio waliokaa darasani, kwenda maktaba na kufanya utafiti, mafanikio yao yametokana na michango ya wadau wengi ikiwa ni pamoja na Serikali,familia, asasi na watu mbalimbali". Amesema Prof.Anangisye.

Kwa Upande wake Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.Stephen Maluka amesema kwa mwaka 2020/2021 Chuo kilitenga Shilingi Milioni 413.5 kwaajili ya mafunzo ya watumishi kati ya kiasi hicho, shilingi milioni 113.5 ni kwaajili ya mafunzo ya muda mfupi na shilingi Milioni 300 kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu.

Amesema Chuo kilitenga shilingi Milioni 300 katika bajeti ya mwaka 2020/2021 kiasi ambacho kinatarajiwa kuongezeka kila mwaka kadri itakavyowezekana.

"Shughuli za kiutafiti zimeenda sambamba na kuongezeka kwa machapisho yanayotolewa na wanataaluma wa Chuo. Ili kuimarisha shughuli za kitafiti, jarida la Chuo liitwalo Journal Of Education, Humanities and sciences, ambalo lilipata hadhi ya Kimataifa mwaka 2017 limeendelea kuchapishwa kwa wakati na hivyo kuwavutia wanataaluma wengi ndani na nje ya nchi kuchapisha matokeo ya tafiti ". Amesema Prof.Maluka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments