MRADI WA KUHIFADHI MISITU KUPITIA BIASHARA ENDELEVU YA MAZAO YA MISITU YANUFAISHA WANANCHI KIJIJI CHA IHOMBWE, MIKUMI MOROGORO

 

Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge akizungumza katika mkutano wa utoaji wa taarifa kwa waandishi wa habari na maafisa wa Shirika la TFCG ambao wapo katika ziara ya kukagua mradi wa uhifadhi mazingira inayotekelezwa mkoani hapa. Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ihombwe, Uashty Chimile

Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG Elida Fundi  akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa Kamati Mpya ya Maliasili Agatha Gambe akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Mtandao wa Wazalishaji Mkaa kwa njia  Endelevu wa Wilaya ya Kilosa Kulangwa Ganda akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Enyasi Simon akizungumza kwenye mkutano huo.
Philemoni Robert akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa Kamati ya Maliasili wakiwa kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja.
 
MRADI wa Kuhifadhi Misitu kupita biashara Endelevu ya mazao ya misitu unaotekelezwa na Shirika la  Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu (MJUMITA)kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC) umewanufaisha Wananchi  wa  Kijiji cha Ihombwe kilichopo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mikumi mkoani Morogoro  kwa kukamilisha 
miradi kadhaa ya maendeleo.
 
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Vashty Chimile wakati akitoa taarifa kwa  waandishi wa habari na maafisa wa Mradi ambao wapo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji  wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu mkoani hapa.
 
Chimile alielezea mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa shighuli za usimamizi wa nMisitu kijiji hapo ikiwemo utekelezaji wa  miradi mbalimbali ya maendeleo  kutokana na fedha  zinazotokana na tozo za uzalishaji wa mazao ya Misitu kwa njia Endelevu ambao o hapo awali kabla  ya mradi huo walikuwa hawazipati.
 
Alisema mradi huo katika kijiji hicho ulianza Mwaka 2012 kwa kuanza kutengeneza mipango ya  matumizi bora ya ardhi na mipango ya usimamizi wa Misitu na kupatiwa mafunzo mbalimbali. Kijiji  kiliaanza kuvuna na kuingiza kipato mwaka Julai 2014 ambapo mapato ya kwanza yalikuwa ni zaidi ya  Sh.33.5 Milioni na hadi kufikia mwaka 2021 walikuwa wamekusanya zaidi ya Sh.259.Milioni.
 
Alisema mpaka sasa fedha zilizotumika ni zaidi ya Sh.189 Milioni na benki zipo Sh. 70 milioni  mbazo zimefanyiwa mpango wa matumizi mpaka mwaka wa fedha wa 2021/2022.
 
Alitaja matumizi ya fedha hizo kuwa wameweza kuchonga  barabara ya kilomita tisa, ujenzi wa  madarasa matatu ya shule ya Msingi kwa Sh.45 milioni, uchimbaji wa kisima cha maji cha mita 121  kwenda chini na kujenga nyumba ya mganga wa zahanati ya kijiji, kujenga vyoo katika nyumba za  watumishi wa Serikali waliopo kijijini hapo, kuweka umeme katika ofisi zote za taasisi za Serikali, kununua baadhi ya vifaa katika wodi ya wazazi wa zahanati hiyo na mwaka 2014/ 2015  walifanikiwa kuwalipia bima ya afya wananchi wote wa kijiji hicho.
 
Mkazi wa Kijiji hicho Philemon Robert alisema kabla ya kuanza mradi huo kulikuwa na uharibifu  mkubwa wa misitu ya ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa na mbao laking baada ya  kuanza mpango huu wa Usimamizi shirikishi wa Misitu na biashara Endelevu ya mazao ya Misitu  wamepata mafanikio makubwa ya kukusanya mapato mengi kutokana na kuuza mkaa endelevu na mbao.
 
Afisa Uhusiano wa TFCG Bi, Bettie Luwuge aliwaomba wananchi wa kijiji hicho kuwapa ushirikiano  wajumbe wa kamati mpya ya maliasili iliyochaguliwa hivi karibuni ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi zaidi.
 
 Afisa Sera na Majadiliano wa MJUMITA Elida Fundi alisema usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii  ni dhana ambayo ikitekelezwa vizuri zaidi itasaidia wananchi kupata maendeleo yao na kuokoa  misitu ambayo inaendelea  kupotea kwa kiwango kikubwa kwenye ardhi ya vijiji isiyokuwa chini ya  usimamizi maalumu.
 
Katibu wa Mtandao wa Wazalishaji Mkaa kwa njia  Endelevu wa Wilaya ya Kilosa Kulangwa Ganda  alisema mafunzo mbalimbali waliyopewa na mashirika haya yamesaidia sana kutekeleza shuhguli za  Usimamizi wa Misitu ya jamii vizuri. Mafunzo haya yamewasaidia kuelewa wajibu wao wa utumzaji wa  Misitu badala ya kuwachia serikali hasa dhana iliyojengeka kwa wananchi kuwa anayepaswa kuilinda  ni Serikali na kuwa sasa mapato yameanza kuonekana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments