Breaking

Post Top Ad

Sunday, November 21, 2021

ASKARI POLISI AUAWA KWA KUCHOMWA MSHALE AKIFUATILIA MWIZI WA MAHINDI SHAMBANIMaafisa wa polisi katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet nchini Kenya wameanzisha msako wa kumsaka mwanamume anayedaiwa kumuua askari kwa kumdunga kichwani mshale wenye sumu.

Eliud Kipkosgey anakabiliwa na tuhuma za kumuua Julias Mengich Kipserem, polisi anayehudumu katika kituo cha Polisi cha Kapsowar, Ijumaa, Novemba 19,2021.

 Taarifa ya polisi ilisema kuwa afisa huyo alikuwa na wenzake kutoka ambao walikuwa wakifuatilia malalamishi yake Wesley Biwott Chemisto kwamba jamaaa mmoja aliyetambulika kama Adams alikuwa akiiba mahindi yake shambani. 

"Iliripotiwa na Morrison Ndung'u Konstebo wa Kituo cha Kaptabuk kwamba leo karibu saa kumi jioni akiwa ameshika doria katika eneo la Koinarak kilomita 5 Kusini-Mashariki mwa kituo hicho alipata malalamishi kutoka kwake Wesley Biwott Chemisto kumhusu Adams ambaye alikuwa akivuna mahindi yake,” ripoti hiyo ilisema.

Ni wakati wa msako huo ambapo mshukiwa alianza kumpiga afisa huyo akamuangusha chini kabla ya kuchomoa mshale wake wenye sumu na kumdunga. 

Kisa hicho kiliwalazimu maafisa wengine kuacha misheni yao na badala yake kumkimbiza mwenzao aliyejeruhiwa hospitalini. 

Afisa huyo alipelekwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Chebiemit kabla ya kuhamishwa hadi Hospitali ya Rufaa ya Moi.

 Hata hivyo, alithibitishwa kwamba tayari amekata roho alipofikishwa katika hospitali hiyo iliyoko mjini Eldoret.

 Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika makafani ya Rufaa ya Moi kusubiri upasuaji ambao umepangwa kufanyika Jumatatu, Novemba 22.

 Eneo la uhalifu ambapo Kipserem alidungwa lilitembelewa baadaye na maafisa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi wa Jinai Marakwet Magharibi na OCS wa Kituo cha Polisi cha Kapsowar.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages