LUNGUYA, SHILELA WAFUNGUKA MATUNDA YA TGNP KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA.... NDABA ATAKA UTAYARI NA NGUVU YA KUZUIA UKATILI


Afisa Programu Ujenzi wa Nguvu za Pamoja na Harakati wa TGNP, Florah Ndaba akizungumza katika kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Afisa Programu Ujenzi wa Nguvu za Pamoja na Harakati wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Florah Ndaba amewataka watu wote katika jamii kuzuia matukio ya ukatili wa kijinsia kutokana na kwamba kesi za matukio hayo zinamaliza muda mwingi na rasilimali fedha.

Ndaba ametoa rai hiyo Novemba 20,2021 kwenye kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga kilicholenga kufanya Tathmini za harakati zao katika kutekeleza mradi kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na TGNP kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Umoja la Idadi ya watu (UNFPA)

Kikao hicho kimekutanisha watu maarufu katika kata ya Lunguya wakiwemo viongozi wa jeshi la jadi sungusungu,wazee wa mila ,vijana, wanaume, wanawake, viongozi wa dini,siasa,wafanyabiashara, wakulima, maafisa watendaji wa vitongoji, vijiji na kata, vituo vya taarifa na maarifa,Wasaidizi wa Kisheria,Jeshi la polisi ambao kwa pamoja wameeleza mafanikio,changamoto na hatua wanazochukua katika kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Afisa Programu Ujenzi wa Nguvu za Pamoja na Harakati TGNP, Florah Ndaba amesema TGNP inaendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) huku akibainisha kuwa ni Jukumu la kila mmoja katika jamii.

“Ulinzi wa Jamii ni jukumu la kila mmoja katika jamii, Mtatuzi wa changamoto zetu ni sisi wenyewe. Tunataka watoto wanaozaliwa wakikua wasikutane na changamoto ambazo wewe hivi sasa unakutana nazo. Ili kutekeleza haya ni lazima kila mmoja awe na utayari wa kuleta mabadiliko”,amesema Ndaba.

“Kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia zinachukua muda mwingi na rasilimali fedha nyingi ndiyo maana wengine wanaamua kuzimaliza kifamilia. Naomba muangalie sana suala la kuzuia matukio ya ukatili ya kijinsia na ili kufanikisha haya ni lazima sote kupitia makundi mbalimbali tushirikiane kuondoa changamoto zilizopo. Kila mmoja ana mchango, kama kuna mfumo dume tukae tujadili namna ya kuuondoa ili tuishi kwa amani na upendo”,ameongeza Ndaba.

Katika hatua nyingine amevipongeza vituo vya taarifa na maarifa Lunguya na Shilela kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kuibadili jamii na kuwa na nguvu ya pamoja katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia na kufanya shughuli za maendeleo huku akibainisha kuwa harakati wanazozifanya katika kujitolea kuleta mabadiliko ni maisha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija amesema harakati zinazofanywa na Wana Mabadiliko kwa usimamizi wa TGNP zimeanza kuzaa matunda kwani jamii imetambua madhara ya ukatili wa kijinsia na sasa hata wale washika mila na desturi kandamizi wanashiriki katika harakati za kumlinda mwanamke na mtoto na kuachana na vitendo vya ukatili.

Mzee wa Kimila Maria Stephano Ntoye (68) kutoka kata ya Lunguya amesema TGNP imeleta mabadiliko katika jamii kwa kuondoa mila na desturi kandamizi ambapo sasa wanawake wana sauti na wana uwezo wa kushiriki kujadili maamuzi ndani ya familia na kumiliki mali tofauti na hapo awalia ambapo wanaume ndiyo walionekana kuwa na nguvu zaidi katika familia na jamii.

“Ujio wa TGNP Lunguya na Shilela una faida kubwa sana kwetu, mmetubadilisha pakubwa sana, hivi sasa hata wale Waswezi/Wakango waliokuwa wanacheza ngoma huku wakitoa matusi yanayodhalilisha wanawake sasa wameanza kubadilika”,amesema Bi. Grace.

Naye Mzee Maarufu Thadeo Stephano wanaendelea kutatua migogoro ya matukio ya ukatili wa kijinsia na wanaume wameanza kuachana na mifumo dume inayogandamiza mwanamke na wanawake wameanza kudai haki zao.

Hata hivyo amewasihi wanawake kutotumia nguvu kubwa kudai haki na wajitahidi kuheshimu waume zao badala ya kuwatendea dhambi wanaume kwa kujificha kwenye kivuli cha uanaharakati.

Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya, Irene Ibrahim Nyanza amesema kutokana na elimu waliyopata kutoka TGNP hivi sasa wanajua ni hatua gani za kuchukua nan i mahali gani pa kwenda kupeleka matukio ya ukatili ya ukatili wa kijinsia huku akibainisha kuwa matukio ya ukatili yamepungua.

Naye Mwakilishi wa kundi la wanaume kutoka kata ya Shilela, Amos Daudi amesema kutokana na elimu waliyopewa hivi sasa wanaume wanashirikiana na wanawake katika maamuzi ndani ya familia badala ya wanaume kuwa na waamuzi pekee.

Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lunguya Mhe. Grace Masanja na Diwani wa kata ya Lunguya Mhe. Musa Manuari wamesema wana kila sababu ya kuipongeza TGNP kwani imesaidia kuwafanya wanawake waanze kujiamini na kujisimamia katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Koplo Rajabu Sese kutoka kituo kidogo cha Polisi Lunguya amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la polisi katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa za matukio ya ukatili pamoja na kutoa ushahidi badala ya kuripoti matukio kisha kumaliza kesi kifamilia.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee amesema ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia ni lazima kila mmoja atoe ushirikiano ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa wakati pindi matukio hayo yanayopotokea.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Programu Ujenzi wa Nguvu za Pamoja na Harakati wa TGNP, Florah Ndaba akizungumza katika kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kufanya Tathmini za harakati zao katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kilichoandaliwa na TGNP na UNFPA. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Programu Ujenzi wa Nguvu za Pamoja na Harakati wa TGNP, Florah Ndaba akizungumza katika kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Afisa Programu Ujenzi wa Nguvu za Pamoja na Harakati wa TGNP, Florah Ndaba akizungumza katika kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza katika kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza katika kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee akizungumza katika kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lunguya Mhe. Grace Masanja Kabiliga akizungumza katika kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Koplo Rajabu Sese kutoka kituo kidogo cha Polisi Lunguya akieleza namna Jeshi la polisi linashirikiana na jamii katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye kikao cha Wana Mabadiliko kata ya Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga
Mzee wa Kimila Maria Stephano Ntoye akielezea namna TGNP ilivyoleta mabadiliko katika jamii ambapo sasa wanawake wamezitambua haki zao hivyo kuwa tayari kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika ngazi zinazohusika.
Mzee Maarufu Thadeo Stephano akielezea namna watu maarufu wanashiriki katika mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuepuka mila na desturi kandamizi zinazomnyima haki mwanamke.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya, Irene Ibrahim Nyanza akielezea kuhusu mafanikio waliyofikia katika kutokomeza ukatili wa kijinsia
Diwani wa kata ya Lunguya Mhe. Musa Manuari akizungumza kwenye kikao hicho ambapo alisema jamii sasa imebadilika imeanza kutambua athari za matukio ya ukatili wa kijinsia.
Msaidizi wa Kisheria Esther Mwampashi kutoka kata ya Bulige akielezea hatua wanazochukua katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwa kushirikiana na Vituo vya taarifa na maarifa
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela akielezea mafanikio waliyofikia katika kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kufuatilia wanafunzi watoro shuleni
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya Meja Masalu akielezea mafanikio waliyofikia katika kutokomeza ukatili wa kijinsia
Kijana Edward Furaha kutoka kata ya Lunguya akielezea hatua wanazochukua kama vijana katika kutoa elimu kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia
Kijana Boniphace Alfred kutoka kata ya Shilela akieleza namna wanavyohamasisha jamii kuachana na migogoro ya ndoa
Mwanaume kutoka kata ya Shilela, Amos Daudi akielezea namna wanaume wanavyoshirikiana na wanawake katika maamuzi ndani ya familia badala ya wanaume kuwa na maamuzi pekee.
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Picha ya pamoja baada ya kikao
Picha ya pamoja baada ya kikao

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments