Breaking

Post Top Ad

Friday, October 22, 2021

'MR TANZANIA 2021 KUPATIKANA USIKU WA LEO UBUNGO PLAZA


Na Andrew Chale,  Dar es salaam

JIONI ya leo 22 Oktoba ni hekaheka na mbwembwe za watunisha misuli mbavu katika kumsaka Mshindi Mr Tanzania 2021 tukio litakalofanyika ndani ya Ubungo Plaza.

Kwa mujibu wa Kamati ya mashindano ya MR Tanzania imesema jioni ya leo washiriki wote wa Mr . Tanzania wataonesha uwezo wao katika kinyang'anyiro hicho tukio litakalofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro, Ubungo Plaza Dar es Salaam kuanzia saa 7:00 jioni hadi saa tano usiku.

Awali Katibu Mkuu wa Shirikisho la mchezo huo toka (TBBF ) Francis Mapugilo amesema  wanatarajia shindano litakuwa katika hekaheka tofauti huki washindi wakitarajia kuondoka na zawadi nono.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Pilipili Intertainment Millesh Batt, ambao ndio waandaji washindano hilo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi leo huku kwa wale ambao hawatobahatika kufika ukumbini watalishuhudia kupitia cheneli za Moto tv.

"Ili kununua Tiketi yako kuja kushuhudia MR TANZANIA GRAND FINALE  leo utaipata mlangoni Ubungo Plaza na milango itakuawa wazi kuanzia saa 12 jioni.

Onesho hili limewezeshwa na Mambo Moto na  Mambo TV Swahili." Alisema.

Ambapo amevitaja viingilio vya tiketi kuwa ni pamoja na:

"Elfu 25,000 (REGULAR)
Elfu 50,000 (V.I.P)
Shilingi 100,000 (V.V.I.P).

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages