KIJANA AUAWA BAADA YA KUTOROSHA BINTI NA KUMTAMBULISHA KAMA MKE BILA KUTOA MAHARI SINGIDA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, October 9, 2021

KIJANA AUAWA BAADA YA KUTOROSHA BINTI NA KUMTAMBULISHA KAMA MKE BILA KUTOA MAHARI SINGIDA

  Malunde       Saturday, October 9, 2021

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Stella A. Mutabihirwa

Na Edina Malekela,Singida.
Kijana aliyejulikana kwa jina Nchimwa Magidu Ndula (22) mkazi wa Madalawa amefariki dunia baada ya kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake mzazi aitwaye Magidu Ndula Jisusi (55) baada ya kijana huyo kumtorosha binti aliyetaka kumuoa na kumpeleka kwao kama mke bila ya kufuata taratibu za kutoa mahari.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Stella Mutabihirwa tukio hilo limetokea Oktoba 8, 2021 majira ya saa 10 alfajiri katika kitongoji cha Madalawa kijiji cha Mlandala kata ya Urughu wilaya ya Iramba mkoani Singida.

 "Nchimwa Magidu Ndula (22) mkazi wa Madalawa alifariki dunia baada ya kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake mzazi aitwaye Magidu Ndula Jisusi (55) mkazi wa Madalawa",amesema Kamanda Mutabihirwa.

"Jeshi la polisi limefanya uchunguzi wa awali na kubaini kuwa marehemu alipigwa akiwa nje ya nyumba yao alipokuwa anaishi na wazazi wake huku chanzo cha tukio hilo kikibainika kuwa ni mgogoro wa kifamilia uliopelekea kutoelewana baina ya marehemu na mtuhumiwa baada ya marehemu kumtorosha binti aliyetaka kumuoa kutoka kwenye himaya ya wazazi wake na kumpeleka kwao kama mke bila ya kufuata taratibu za kutoa mahari kama mila za kabila la Wasukuma linavyotaka",amefafanua.

Amesema tayari Jeshi la polisi la Polisi mkoa wa Singida linamshikilia Magidu Ndula Jisusi (55) kwa mahojiano zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Kamanda Mutabihirwa ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani vitendo hivyo vinasababisha uvunjivu wa amani na wakati mwingine kusababisha vifo

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post