TEKSI ZAGEUKA MASHAMBA YA MBOGA MBOGA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, September 20, 2021

TEKSI ZAGEUKA MASHAMBA YA MBOGA MBOGA

  Malunde       Monday, September 20, 2021

Katika maegesho ya gari nchini Thailand katika mji mkuu wa Bangkok, utaona mbogamboga zikiwa zimeota katika paa ya magari ya kukodi ambayo yana rangi mbalimbali za kung’aa.

Vizuizi vikali vilivyowekwa nchini Thailand dhidi ya Covid-19 vimesababisha mji huo ambao ulikuwa na hekaheka nyingi kuwa na utulivu, na kufanya madereva wa teksi kukosa kazi.

Baada ya kukosa wateja, madereva wengi waliondoka mjini na kwenda nyumbani kwao vijijini, na kuacha kile kilichoitwa makaburi ya taksi.

Je, kazi hizi zinatokomea?

Na sasa kampuni moja imeamua kutumia paa za magari hayo ambayo hayafanyi kazi kama shamba la kulimia mbogamboga, ambapo wanatarajia wanaweza kusaidia kuwalisha madereva na wafanyakazi wengine.

Wafanyakazi wa taksi za ushirika wa Ratchaphruek wametengeneza bustani ya mbogamboga kwa kuweka udongo juu ya karatasi nyeusi za plastiki.

Wamepanda mbegu mbalimbali za mboga kama pilipili , matango na zukini. Wana matumaini kuwa baada ya kuwasaidia madereva, chakula chochote kitakachosalia kitauzwa sokoni.
Biashara ya taksi mjini Bangkok kwa kawaida inategemea utalii katika sehemu kubwa lakini marufuku yaliyowekwa ya kuzuia wageni kuingia nchini humo ina maana kuwa karibu kila kitu kimesimama.

“Hili ndilo chaguo letu la mwisho,” Thapakorn Assawalertkun, mmoja wa wamiliki wa kampuni aliwaambia wakala wa habari AFP, aliongeza kusema kuwa magari mengi yana mkopo mkubwa bado ambao hawajamaliza kulipa.

“Kuotesha mboga za majani katika paa la taksi hakutaharibu magari hayo kwa kuwa kuna mengine ambayo yameshaharibika na hayawezi kutengenezeka . Kuna ambayo yameharibika injini, hayana matairi, hakuna kitu kinaweza kufanyika,” alisema.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post