TAFIRI TAFIRI YATAKIWA KUFANYA KAZI YENYE TIJA KWENYE SEKTA YA UVUVI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, September 7, 2021

TAFIRI TAFIRI YATAKIWA KUFANYA KAZI YENYE TIJA KWENYE SEKTA YA UVUVI

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja katika makao makuu ya taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam na kuwataka wafanyakazi hao kufanya kazi yenye tija kwa jamii kupitia sekta ya uvuvi. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei akifafanua namna taasisi hiyo inavyokabiliwa na changamoto ya vifaa vya maabara vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5 mara baada ya jengo la maabara kukamilika. Dkt. Kimirei amebainisha hayo wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki aliyofanya katika makao makuu ya taasisi hiyo. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).
Mratibu wa Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi Bw. Nichrous Mlalila akifafanua namna mradi huo wa miaka sita hapa nchini unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, ulivyoweza kuleta tija katika sekta ya uvuvi nchini kupitia tafiti na elimu. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akikagua jengo la maabara la Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) lililojengwa kupitia Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH), ambapo Waziri Ndaki amesema atahakikisha jengo hilo linapata vifaa vya maabara vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5 ili lifanye kazi iliyokususdiwa. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), (Kulia) akibadilishana mawazo na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH), Bw. Nichrous Mlalila (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, mara baada ya Waziri Ndaki kufanya ziara ya kikazi ya siku moja katika makao makuu ya TAFIRI. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).
Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH), Bw. Nichrous Mlalila pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAFIRI, mara baada ya Waziri Ndaki kufanya ziara ya kikazi ya siku moja katika makao makuu ya TAFIRI. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).


 Na. Edward Kondela

 

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) imetakiwa kufanya kazi zenye tija kwa jamii na kutoa ushauri wa kisayansi namna ya kuhakikisha sekta ya uvuvi inakua na kusaidia watanzania katika masuala ya uvuvi

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) amebainisha hayo jana (06.09.2021) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika makao makuu ya taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa TAFIRI inategemewa katika kufanya tafiti za uvuvi kwa manufaaa ya sasa na yajayo na kuwafanya wavuvi kuwa na kipato endelevu ili shughuli hiyo ifanywe kitaalamu.

Aidha, amepongeza Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH), ambapo umewezesha kujengwa kwa jengo la maabara ya TAFIRI ambalo litaongeza wigo katika kufanya tafiti za uvuvi hapa nchini.

Amefafanua kuwa SWIOFISH imekuwa ikifanya kazi ya msingi na muhimu nje ya nchi na kuhakikisha fedha ambazo zimetolewa na Benki ya Dunia katika mradi huo zinasimamiwa vyema na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI Dkt. Ishmael Kimirei amemwambia Waziri Ndaki juu ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo zikiwemo za vifaa vya maabara baada ya jengo la maabara kukamilika ambapo amesema vifaa hivyo vinagharimu Shilingi Bilioni 1.5.

Kutokana na ukosefu wa vifaa vya maabara, Waziri Ndaki amemhakikishia mkurugenzi huyo kuwa, ataliwekea uzito jambo hilo kuanzia sasa na mwaka ujao wa fedha ili vipatikane vifaa hivyo na jengo hilo lifanye kazi ya utafiti pekee badala ya kuwa na vyumba vya ofisi.

Naye Mratibu wa mradi wa SWIOFISH Bw. Nichrous Mlalila amesema mradi huo wa miaka sita hapa nchini unaotarajia kufikia tamati mwezi Septemba mwaka 2022, umefadhiliwa na Benki ya Dunia na lengo la mradi ni kusimamia masuala ya uvuvi kuanzia ngazi ya utawala hadi kwa wavuvi pamoja na ushirikiano kwa kikanda katika kuhakikisha unaboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages