MWANAMKE AUAWA AKITUHUMIWA KUWA MCHAWI ANAROGA NG'OMBE WANAPOTEA



Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Mwalu Charles (45) mkazi wa kijiji cha Shilabela kata ya Ulewe wilayani Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za mgongoni, kichwani na mkono wa kulia akituhumiwa kuwa mchawi na watu wanaotafutwa na Jeshi la polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9,2021 majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Shilabela, kata ya Ulewe, tarafa ya Mweli ,wilaya ya kipolisi Ushetu, wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga.

“Mwalu Charles (45) mkazi wa kijiji cha Shilabela, alikufa kwa kukatwa na kitu chenye makali sehemu za mgongoni, kichwani na mkono wa kulia na watu au mtu wanaotafutwa”,amesema.

Amesema kiini cha tukio ni mgogoro wa kifamilia unaochochewa na imani za kishirikina ambapo marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa mchawi.

"Chanzo cha tukio hili ni mgogoro wa kifamilia hiyo kwamba huyo mama anaroga ng'ombe wanapotea, kwa hiyo wakawa wanamtuhumu kuwa anaroga wanapotea ndiyo wakamfanyia kitendo hicho",ameeleza Kamanda Kyando.

"Katika Upepelezi na Uchunguzi wa awali tumekamata watuhumiwa watatu wa familia hiyo hiyo waliokuwa wanachukua ng'ombe wa familia na kwenda kuuza halafu wanamwambia mzee wao kwamba huyo mama 'shemeji yao' anaroga ng'ombe wanapotea",amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments