MO DEWJI: HANS POPE ALIKUWA NA WEMA WA KIPEKEE | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 11, 2021

MO DEWJI: HANS POPE ALIKUWA NA WEMA WA KIPEKEE

  Malunde       Saturday, September 11, 2021


Na Emmanuel Mbatilo - Dar es salaam
Wanamichezo nchini wamepokea kwa masikitiko kwa kifo cha Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Zacharia HansPope ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Aghakhan Jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.

Viongozi mbalimbali wa michezo wameshindwa kujizuia na kutamka ya moyoni kuhusu umuhimu wa kiongozi huyo katika tasnia ya michezo hapa nchini.

Licha ya kuwa kiongozi wa klabu ya Simba alikuwa mtu wa hamasa katika kuitangaza tasnia ya michezo kwa taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji amesema Hans Pope alikuwa ni mtu wa kipekee alihakikisha klabu ya Simba kusonga mbele na alijali maslahi ya klabu.

“Nimefanya kazi na wewe kwa miaka mingi, na kila siku uliweka maslahi ya Simba mbele. Kaka yangu ulikua na wema wa kipekee, na ulikua wa kwanza na ulinyooka linapokuja suala la kuilinda Simba, hukuwa na maslahi binafsi. Ulikua rafiki wa marafiki wa Simba, na ulikua tofauti na wasioitakia mema Simba.” Amesema Mo Dewji

Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amesema Hans Pope alikuwa anapenda umoja na mshikamano kwa wanasimba wote kwani alikuwa anapenda mafanikio kwa ujumla ndani ya klabu.

“Ninamfahamu kwa miaka mingi akiwa ni Mwana Simba mahiri , mwenye msimamo na ukweli. Ni mtu aliependa umoja na kupata mafanikio kwa jumla. Siku zote alikubali kutumikia klabu kwa moyo wake wote , bila kujali muda wake, mali au hasara”. Amesema Mangungu
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post