WANAFUNZI WAMTEMBEZEA KICHAPO MWALIMU WAO



Wanafunzi watatu wa kidato cha nne katika shule ya upili/sekondari ya St John Sikinwa kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya wamemvamia na kumpiga mwalimu wao wa Hisabati nyumbani kwake. 

Nicholas Bett ambaye ni mwalimu wa taasisi hiyo iliyoko eneo la Saboti alishambuliwa nyumbani kwake na wanafunzi hao majira ya saa moja unusu alasiri.

Walivamia makazi yake ambayo yapo mkabala na bweni la shule hiyo kulingana na ripoti ya TV 47. 

Waliripotiwa kumpiga Bett kwa kifaa butu shingoni na baada ya hapo, wakaanza kumyeshea ngumi na mateke wakati walipomzidi nguvu.

 Waliripotiwa kumpiga Bett kwa kifaa butu shingoni na baada ya hapo, wakaanza kumnyeshea ngumi na mateke wakati walipomzidi nguvu. 
Inaarifiwa kwamba mzozo uliibuka wakati wanafunzi hao walikuwa wakilipiza kisasi kwa kumshambulia mwalimu huyo ambaye aliwasisitizia ni sharti wapendezwe na masomo yake. 

Walimu wengine wawili ambao wanaishi katika kiwanja kimoja na mwathiriwa walifanikiwa kutoroka jaribu hilo bila kujeruhiwa. 

John Naibei na Michael Odhiambo walitoroka baada ya majirani kupiga kamsa na kuwalazimu wanafunzi hao kuhepa. 

Naibei na Odhiambo walipiga ripoti katika Kituo cha Polisi cha Gituamba wakishinikiza kukamatwa kwa wanafunzi hao watoro. Wanataka pia wanafunzi hao washtakiwe kortini.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Walimu wa Shule za Msingi (KUPPET) tawi la Trans-Nzoia Furaha Lusweti alitoa wito kwa Tume ya Kuajiri Walimu kuwahamisha walimu hao watatu.

 Wanafunzi hao watatu wangali mafichoni na tangu Jumatatu hawajaonekana shuleni. 

Tangu mwaka wa 2021 kuanza, kumekuwa na ongezeko la mizozo ya walimu na wanafunzi huku kisa hiki kikiongezea tu katika takwimu hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments