SERIKALI YAAGIZA WANAOKASHIFU VIONGOZI MITANDAONI WAKAMATWE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

SERIKALI  imeviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake kuwakamata na kuwachukulia hatua kali  wanaotumia mitandao ya kijamii   kuwakashifu viongozi wa Serikali na kusema kuwa ni kinyume cha sheria.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene amesema hayo leo jijini Dodoma kwenye mkutano wake na waandishi wa habari huku akisema hali hiyo haitavumilika na kwamba  kuanzia sasa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa wale wote watakao endelea na tabia hiyo.  


Simbachawene  amesema kila mwananchi anapaswa kusimamia matumizi sahihi ya mitandao  ukiwemo wizi unaofanyika pamoja na uhuru wa kutoa mawazo ambao wengi wamekuwa wakiutumia vibaya kwenye mitandao ya kijamii.


"Namuagiza Kamishina wa polisi nchini Camillus Wambura kushughulikia wale wote wenye malalamiko ya kutoa fedha ili kesi zao zishughulikiwe na jeshi la polisi kwenye kesi za makosa ya jinai,"amesema .


Aidha Waziri Simbachawene amebainisha kwamba zaidi ya shilingi milioni 500 hadi Bilioni 1 fedha za wananchi wanyonge, wastaafu huibiwa na matapeli kwa njia ya mitandao .

"Kuna  wananchi hulipishwa fedha pindi wanapoenda kulalamika kupotelewa na vitu vyao ikiwemo simu za mkononi na baadhi ya polisi kuwadai wananchi fedha ,nawaomba polisi  kuacha mara moja tabia hiyo na mkasimamie haki na maadili,"amesisitiza Simbachawene.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post