KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM ATEMBELEA KIWANDA CHA SHINYANGA BEST IRON | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, September 12, 2021

KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM ATEMBELEA KIWANDA CHA SHINYANGA BEST IRON

  Malunde       Sunday, September 12, 2021
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gilibet Kalima (katikati)  kutembelea kiwanda cha Shinyanga Best Iron

Na Suzy Luhende - Shinyanga
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gilibet Kalima akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga ametembelea Kiwanda cha Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini (Makarasha) ya Shinyanga Best Iron, kinachomilikiwa na Kashi Salula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga.

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gilibet Kalima ametembelea Kiwanda hicho Jumapili Septemba 12,2021 akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga ambapo amempongeza Mmiliki wa Kiwanda hicho kwa juhudi za kukiendeleza kiwanda hicho na kumtaka aendelee na juhudi zake ili kiendelee kuhudumia watu wengi nchini.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula amemshukuru Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gilibet Kalima kwa kutembelea kiwanda hicho kwani ameahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi ili kiweze kuwa cha kimataifa.
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gilibet Kalima (katikati aliyeshika mikono nyuma) akiwa katika Kiwanda cha Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini (Makarasha) ya Shinyanga Best Iron, kinachomilikiwa na Kashi Salula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akizungumza wakati Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gilibet Kalima (katikati)  akitembelea kiwanda cha Shinyanga Best Iron
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akimshukuru Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gilibet Kalima kutembelea kiwanda cha Shinyanga Best Iron
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gilibet Kalima  (wa pili kulia) akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha Shinyanga Best Iron
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post