BABU WA MIAKA 92 AMBAYE HAJAWAHI KUHUDHURIA MAZISHI WALA KUKANYAGA KANISANI TANGU AZALIWE AOKOKA

Owuor Nyapoya 
**
Katika miaka 92, ambayo Owuor Nyapoya kutoka Usenge katika kaunti ya Siaya nchini Kenya ameishi, hajawahi kukanyaga kanisani wala kuhudhuria mazishi.

Ni kipindi ambacho mvuvi huyo amekuwa mtu tofauti sana duniani. 

Hata hivyo, hayo yote yalikuja yakabadilika wakati aliamua kwenda katika Kanisa Katoliki la St. Martin na kubatizwa. 

Kwa mujibu wa ripoti ya Sunday Standard, Nyapoya alikuwa amevalia shati nyeupe, longi ya kijivu na viatu vyeusi.

Kulingana na Padri Stephen Ouma, ambaye anasimamia Parokia hiyo, Nyapoya alikuwa mtu mzee zaidi kwake kuwahi kubatiza katika maisha yake yote kama mtumishi wa Mungu.

 Aliishi sana Uganda Nyapoya alifichua kuwa aliamua kubadilisha maisha yake ya kiroho kwa sababu amekuwa na bahati ya kuishi maisha marefu kuwaliko watu wengi.

“Si watu wengi wa umri wangu walifaulu kuishi na Ukimwi kwa sababu ya maisha waliyokuwa wanaishi. Kulikuwa na chakula kingi, pesa na wanawake," alisema. 

Alikumbuka siku za nyuma wakati alipuuza juhudi za familia yake kumshinikiza aokoke.

Nyapoya alifichua kuwa hajawahi kwenda hospitalini na hajiunga na shule kwa sababu baba yake hakuwa anathamini masomo.

 "Tulikuwa tunachunga mifugo ya baba yangu na wakati nilikuwa mtu mzima, niliamua kuwa mvuvi kwa sababu hiyo tu ndiyo ilikuwa shughuli ambayo watu wengi walikuwa wanafanya kuliko ukulima," alisema.

 Ubatizo ulifungua ukurasa mpya katka maisha ya Nyapoya, ambayo itaondoa machungu ambayo alisema yalikuwa yamemjaa moyoni.

 Abatizwa kama Paul

 Kupitia maandiko ya Bibilia, Padri Stephen Ouma alimbatiza Nyapoya kama Paul, na kufungua ukurasa mpya katika maisha yake ya Ukristu.

Padri huyo alisema alimpa jina mpya kulingana na maandiko ya Biblia ambayo huashiria mabadiliko. 

“Paul alikuwa mtenda dhambi lakini aliona mwangaza na alibadilika. Mzee huyu alikubali na hivyo sikuwa na budi bali kumuandaa kwa ufalme wa Mungu," alisema Padri Ouma.

Na sasa akiwa kiumbe kipya, Nyapoya sasa ameanza safari ya Mkristu akijivunia. 

Padri Ouma alisema ilikuwa jambo la kutia moyo kwa mzee wa umri huo kuamua kutafuta wokovu.

 CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments