ALIYEZALIWA NA SEHEMU ZA KIKE KISHA KUOTA SEHEMU ZA KIUME UKUBWANI AOMBA MSAADA


Kijana anayeomba msaada

Kijana wa miaka 19 mkazi wa Bukoba, aliyezaliwa na jinsi ya kike na baadaye kuota sehemu za siri za kiume zilizopelekea sehemu za kike kuzibwa, anaomba msaada wa fedha aende nje ya nchi kuongezwa ukubwa wa maumbile ya kiume, yatakayomwezesha kufanya tendo la ndoa na kuzaa watoto.

Kijana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sasa anavaa mavazi ya kiume na kutumia majina ya kiume aliyoyapata baada ya kula kiapo mahakamani baada ya kukana majina yake ya kike aliyopewa awali mara baada ya kuzaliwa, majina ambayo aliyatumia kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, na kusema anatamani kuoa na kupata watoto.

Mpigie ama tuma mchango wako kupitia namba 0765 135 480 jina ni MAFANIKIO ADELICK KARITUS

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments