BARRICK YATOA MSAADA WA PIKIPIKI KUWEZESHA UKAGUZI WA MIRADI YA KIJAMII WILAYANI NYANG’WALE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 7, 2021

BARRICK YATOA MSAADA WA PIKIPIKI KUWEZESHA UKAGUZI WA MIRADI YA KIJAMII WILAYANI NYANG’WALE

  Malunde       Tuesday, September 7, 2021

Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita , Bw. David William Jamhuri (Kushoto) akipokea msaada wa pikipiki 8 kutoka kwa mrakibu idara ya mahusiano wa Barrick Bulynhulu, William Chungu, zilizotolewa na kampuni kwa ajili ya kuwezesha maofisa wa Serikali wilayani humo kutembelea miradi ya kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Bw. David William Jamhuri (Kulia) akipokea msaada wa pikipiki 8 kutoka kwa mrakibu idara ya mahusiano wa Barrick Bulynhulu, William Chungu, zilizotolewa na kampuni kwa ajili ya kuwezesha maofisa wa Serikali wilayani humo kutembelea miradi ya kijamii
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Bw. David William Jamhuri (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Husna Tonny Chambo pikipiki 8 zilizotolewa na kampuni ya Barrick mgodi wa Bulyanhulu
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita , Bw. David William Jamhuri akijaribu kuendesha moja ya pikipiki zilizotolewa na Barrick.

***
Kampuni ya Barrick imetoa msaada wa pikipiki 8 kwa ajili ya kufanikisha ukaguzi wa miradi ya kijamii wilayani Nyang’hwale iliyopo mkoani  Geita.

Barrick kupitia sera yake ya kusaidia huduma za jamii katika maeneo yanayozunguka maeneo yake ya kazi (CSR), inafadhili miradi mbalimbali ya kijamii wilayani humo.

Msaada huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya hiyo ,David Jamhuri .ilihudhuriwa na wafanyakazi wa Serikali wilayani humo na wafanyakazi waliowakilisha kampuni ya Barrick.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post