MBUNGE SANTIEL KIRUMBA AKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA WASICHANA KISHAPU


Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Kompyuta kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga ili kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi hao. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba amekabidhi vifaa vya TEHAMA zikiwemo Kompyuta 5 , Printa 1 pamoja na spika zake vyenye thamani ya milioni 15 kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga zisaidie kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi hao.

Akikabidhi vifaa hivyo Jana Jumamosi Agosti 14,2021 Mhe. Kirumba amesema kuwa kompyuta hizo zitaenda kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi na kuongeza ufaulu wa shule hizo.

Alisema Kompyuta hizo ni sehemu ya Computer 30 alizoomba kwa kushirikiana na Wabunge wenzake wa Mkoa wa Shinyanga na kutolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Mhe. Kirumba aliishukuru na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara hiyo na taasisi yake ya UCSAF kwa kuthamini na kuisimamia vema ilani ya uchaguzi ambayo imezungumzia kuongeza matumizi ya TEHAMA na wao wanatekeleza kwa vitendo huku akizitaka shule zilizonufaika na vifaa hivyo kuvitunza na kuvitumia kuleta matokeo tarajiwa kwa walimu na wanafunzi wa shule hizo.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude alisema vifaa hivyo vya TEHAMA vitasaidia kuchochea ukuaji wa matumizi ya TEHAMA na kuwaandaa vijana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Mapema Jana Agosti 14,2021 Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew alikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya shule 6 za Sekondari zilizopo ndani ya Mkoa wa Shinyanga ikiwemo shule hiyo ya Kishapu Girls vyenye thamani ya shilingi Milioni 50 vilivyotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Makabidhiano hayo yalifanyika Mkoani Shinyanga kati ya Naibu Waziri huyo na Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Janista Mboneko, na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Shinyanga Nice Munisi ambapo jumla ya kompyuta 30 na printa 4 zilikabidhiwa rasmi.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Kundo alisema kuwa Serikali kupitia UCSAF imeendelea kutekeleza mradi wa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za umma ili kuchochea ukuaji wa matumizi ya TEHAMA na kuwaandaa vijana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Pia alizungumzia mradi wa wasichana na TEHAMA unaotekelezwa na UCSAF ambao unalenga kuwawezesha na kuwajengea uwezo watoto wa kike katika TEHAMA ndio maana katika upelekaji wa vifaa vya TEHAMA katika shule za sekondari Mfuko huo unaangazia na Shule za Sekondari za wasichana.

“Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote tuna kipengele kingine cha kuwawezesha watoto wa kike na TEHAMA ili kuwajengea uwezo na hatimaye kutengeneza wataalam wa TEHAMA wengi zaidi nchini kwa sababu mpaka sasa wataalam wa TEHAMA wanawake ni wachache kuliko wa kiume lengo letu ni kwamba tunapoongelea 50 kwa 50 ionekane kwa vitendo", alisema Mhandisi Kundo.

Kwa Upande wa Mkuu wa Uendeshaji wa UCSAF Mhandisi Albert Richard alisema kuwa vifaa hivyo vya TEHAMA vilivyokabidhiwa katika Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa jumla ya kompyuta 800 na printa 20 zinazoendelea kusambazwa katika ya shule za sekondari za umma ambazo zilianishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/22.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Kompyuta kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga ili kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi hao. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Kompyuta kwa ajili ya sshule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Printer kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Printer kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Wanafunzi wakifuatilia Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments