NAIBU WAZIRI WA MAJI MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI APATA CHANJO YA UVIKO - 19


Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameungana na Watanzania kuitikia wito wa kuchanja chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 zoezi lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu.

Mahundi amepata chanjo hiyo Kituo cha Jakaya Kikwete kilichopiga kambi viwanja vya Farasi Oysterbay mara baada ya mbio za Marathon leo asubuhi zilizoongozwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ambapo pia imewekwa kambi ya kutoa chanjo.

Aidha Waziri Mkuu amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuuweka mwili katika hali ya utimamu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post