RAIS SAMIA APONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI




Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akiwasha umeme katika Shule ya Msingi Mongahay iliyopo Kata ya Tumati wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa huo. Tukio hilo lilifanyika Agosti 14, 2021. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria Makota (katikati), Mbunge wa Mbulu Vijijini, Fratei Massay (mwenye kofia) na Mbunge wa Mbulu Mji, Zacharia Issaay (kulia).


Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani).


Mbunge wa Mbulu Mji, Zacharia Issaay akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani).


bunge wa Mbulu Vijijini, Fratei Massay akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani).


Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria Makota akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani).


Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara, wakati wa Hafla ya Uzinduzi rasmi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa huo.


Kutoka kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri wa Nishati Mhandisi Ngereja Mgejwa, Msimamizi wa Miradi ya Umeme Vijijini Kanda ya Kaskazini kutoka Wizara ya Nishati Mhandisi Shukurani Rugaimukamu na Kaimu Meneja Usimamizi na Uendelezaji Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Emanuel Yessaya wakiwa katika Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani).


Msimamizi wa miradi ya usambazaji umeme vijijini, Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Gilbert Furia (wa tatu-kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Julian Kiiza (kulia) na Kassongo Rubeya (kushoto, mara baada ya Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani) kuzindua rasmi Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Tukio hilo lilifanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021. Wengine pichani ni wafanyakazi kutoka TANESCO.?

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mongahay iliyopo Kata ya Tumati wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara wakitumbuiza kwa kucheza ngoma wakati wa Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa huo. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato.

…………………………………………………………………………………..

Veronica Simba na Zuena Msuya – Manyara

Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, Wabunge wa Majimbo yaliyopo Wilaya ya Mbulu na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sezaria Makota, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kwa utekelezaji makini wa miradi ya umeme vijijini.

Walitoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili katika Mkoa wa Manyara, iliyofanyika Agosti 14 mwaka huu, kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, wilayani Mbulu.

Akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua rasmi Mradi huo, Naibu Waziri Byabato alisema kuwa Rais Samia, kupitia Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza, amewezesha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha vijiji vyote ambavyo havijafikishiwa umeme vinapelekewa nishati hiyo kabla ya Desemba 2022.

Byabato alitumia jukwaa hilo kutoa rai kwa wananchi kuchangamkia fursa ya kufikiwa na miundombinu ya umeme katika maeneo yao kwa kuhakikisha wanalipia shilingi 27,000 tu ili waunganishiwe na kuutumia katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuboresha maisha yao.

“Mheshimiwa Rais ametuwezesha tukawaletea umeme, niwaombe Waheshimiwa Wabunge mhamasishe wananchi wenu wakimbilie fursa hii ili iwaletee maendeleo.”

Akifafanua, Naibu Waziri alieleza kuwa katika baadhi ya maeneo ambayo yaefikishiwa miundombinu ya umeme, mwitikio wa wananchi kulipia ili kuunganishiwa nishati hiyo, umekuwa mdogo, jambo alilolielezea kuwa ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.

“Serikali inatumia gharama kubwa kuhakikisha miundombinu ya umeme inatufikia. Sasa, miundombinu ikifika kwenye maeneo yetu, tuhakikishe sisi sote tunahamasishana kuchangamkia fursa hiyo,” alisisitiza Naibu Waziri Byabato.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria Makota alipongeza kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kusambaza umeme vijijini huku akitilia mkazo kuwa vijiji vyote vya Wilaya hiyo, ambavyo havijafikiwa na umeme, vimeingia katika kufikishiwa nishati hiyo kupitia Mradi huo uliozinduliwa siku hiyo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mji, Zacharia Issaay alieleza kuwa kazi ya kusambaza umeme vijijini iliyofanywa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni ya kupongezwa sana kwani imesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya wananchi.

“Nichukue nafasi hii kuipongeza sana Serikali ya Awamu ya Tano na ya Sita kwa kazi kubwa ya usambazaji umeme vijijini kupitia REA.”

Mbunge Issaay alibainisha kuwa kadri umeme unavyounganishwa katika maeneo mbalimbali ndivyo wananchi wengi wanavyohamasika kufungua miradi ya kimaendeleo zikiwemo mashine za kusaga nafaka, hivyo akaiomba Serikali kuongeza wigo wa upelekaji huduma hiyo kwa manufaa ya jamii husika.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Fratei Massay alimwomba Naibu Waziri Byabato kufikisha salamu za wananchi wa eneo hilo alizoziita ‘za kindakindaki’ kwa Rais Samia kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kuwapelekea maendeleo ikiwemo umeme.

“Naishukuru Serikali kwenye Bajeti hii iliyopita, tumepata vijiji karibu vyote kasoro kimoja tu. Ukikosa kimoja haulalamiki bali unashukuru,” alisisitiza Masai.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga alibainisha kuwa Mkoa wa Manyara una jumla ya vijiji 441 ambapo vijiji 278 tayari vina umeme na vilivyosalia 163 vinapelekewa nishati hiyo kupitia Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili.

Kwa upande wa Wilaya ya Mbulu, Mhandisi Maganga alieleza kuwa kuna jumla ya vijiji 110 ambapo vyenye umeme ni 48. Alifafanua kuwa vijiji vitakavyopelekewa umeme kupitia Mradi huo wa Awamu ya Pili ni 62 na kwa gharama ya shilingi bilioni 18.8.

Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara unatekelezwa na Kampuni ya Ukandarasi ya Nakuroi Investment pamoja na Giza Cable Industries Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 65.3.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments