DC MBONEKO AKAGUA UJENZI DARAJA LA IWELYANGULA, AKEMEA WANAOLIMA KANDO KANDO YA BARABARA

 


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Iwelyangula ambalo linaunganisha Kata za Chamaguha na Kitangili.


Na Marco Maduhu - Shinyanga


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kilimo kandokando ya barabara, hali ambayo inasababisha uharibifu wa miundombinu hiyo yakiwemo Madaraja.

Mboneko ametoa onyo hilo leo Jumanne Agosti 31, 2021wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Iwelyangula, ambalo linaunganisha Kata mbili za Chamaguha na Kitangili zilizopo Manispaa ya Shinyanga.

Amesema ni marufuku wananchi kufanya shughuli za kilimo kandokando ya miundombinu ya barabara, bali walime kwenye maeneo ya mashamba ili kuzuia uharibifu wa miundombinu hiyo, ambayo imekuwa ikiigharimu Serikali kwa kutumia fedha nyingi za matengenezo, ambazo zinge elekezwa kwenye miradi mingine ya maendeleo.

“Ni marufuku wananchi kulima kando ya barabara, kalimeni huko kwenye Mashamba, mnatuharibia barabara zetu na kuingiza gharama Serikali, naagiza pia viongozi wa maeneo haya, wananchi ambao wamelima Kando ya Barabara hii, wavume mazao yao na wasilime tena ili kuilinda barabara na daraja hili,”amesema Mboneko.

“Mwezi wa Sita mwaka huu, nilifika kwenye hili daraja na kukuta limebomoka, na wananchi wa kata hizi mbili za Chamaguha na Kitangili kukosa mawasiliano, ndipo nikapiga Simu kwa Mtendaji Mkuu wa TARURA na kupewa Shilingi milioni 428 kwa ajili ya kujenga daraja jipya ambalo ni bora zaidi,”ameongeza Mboneko.

Aidha Mboneko amesema mbali na ujenzi wa daraja hilo, pia TARURA wameamua kujenga na miundombinu ya barabara Kilomita 1.6 kwa kiwango cha Changalawe, ambayo inaunganisha Kata hizo mbili za Chamaguha na Kitangili kupita kwenye daraja hilo jipya.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi, amesema ujenzi wa daraja hilo ulianza June utakamilika Septemba 30 mwaka huu.

Nao baadhi ya wananchi wa Kata hizo mbili akiwemo Bahati Samali, wamempongeza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, kwa kuwasaidia ujenzi wa daraja hilo, ambalo ni kiungo chao muhimu katika shughuli za kiuchumi, na kupata huduma za afya.

Pia, wanafunzi ambao wanaishi Chamaguha na kusoma Kitangili, ambao huvuka daraja hilo akiwemo Agnes Dotto, wamesema kipindi cha masika hulazimika kubaki nyumbani kwa sababu ya kuhofia kusombwa na maji, lakini daraja hilo litakapokamilika hawatakosa tena vipindi vya Masomo.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja Jipya ambalo linaunganisha Kata ya Chamaguha na Kitangili.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na baadhi ya wananchi wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo na kuwaonya kulima kando kando ya barabara.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumzia ujenzi wa daraja hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa na baadhi ya viongozi kwenye daraja hilo.

Ukaguzi maendeleo ujenzi wa daraja ukiendelea.

Ukaguzi maendeleo ujenzi wa daraja ukiendelea.

Muonekao wa daraja la Iwelyangula, ambalo linaunganisha Kata za Chamaguha na Kitangili.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Daraja.

Ukaguzi wa daraja na Miundombinu ya barabara ukiendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, kushoto akiwa na Diwani wa Chamaguha Elias Masumbuko, wakibadilishana mawili matatu, wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.

Diwani wa Chamaguha Elias Masumbuko, akielezea umuhimu wa daraja hilo, hasa katika masuala ya kukuza uchumi.

Diwani wa Kitangili Manispaa ya Shinyanga Mariam Nyangaka, akizungumzia umuhimu wa daraja hilo, ambalo linaunganisha Kata za Chamaguha na Kitangili.

Mwananchi Bahati Samali, akitoa pongeza kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kuwasaidia ujenzi wa daraja hilo.

Awali Meneja Wakala wa Barabara Mjini na vijijini TARURA Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi, akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, awali akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya barabara na ujenzi wa daraja jipya ya Iwelyangula, ambalo linaunganisha Kata za Chamaguha na Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, Shinyanga







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments