NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. MOLLEL AWATAKA WATANZANIA KUIPA UMUHIMU CHANJO YA UVIKO 19 NI SALAMA


 
Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Godwin Mollel

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Godwin Mollel amewataka wananchi kuipa umuhimu chanjo ya UVIKO-19 na kusema kuwa ni salama kwa afya zao.


Dkt. Mollel amesema hayo leo  Jijini Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa wadau wa huduma za elimu ya afya kwa umma uliofanyika jijini Dodoma ambapo amesema  wananchi hawapaswi kuogopa maneno yanayoendelea mitandaoni kuhusu chanjo hiyo kwani Serikali inawajali na kamwe haiwezi kuwaangamiza.

Mbali na hayo amesema Tanzania ni taifa la Mungu hivyo hatma yake iko mikononi kwa Mungu na kuwataka watanzania kuelekeza imani yao kwa Mwenyezi Mungu kumaliza wimbi la tatu la Ugonjwa huo.

Dk. Mollel ametumia nafasi hiyo  kuwataka  wadau hao wa huduma za elimu ya afya nchini,kuchapa kazi na kuwasihi waandishi kuzingatia maudhui yanayofaa kurusha kwenye vyombo vya habari.

"Msiogope yanayoendelea mitandaoni na kwenye vyombo vya habari ni kawaida tu, mambo yatakaa vizuri,,, Mkachape kazi hayo mengine mtuachie sisi Maronaldo wenu wao watakuja na wataondoka wakiwa wamefunga goli 0,,hali ya chanjo inaenda vizuri", amesema.

Katika kutoa elimu kwa umma aliwataka wadau hao kuwashirikisha watu maarufu, wasanii na viongozi wa dini ili kufikisha elimu kwa umma kuhusu umuhimu a chanjo ya Uviko 19 hasa katika sehemu za vijijini.

Aidha aliwataka wadau kutokujielekeza katika kufanya semina na makongamano na badala yake bajeti iliyowekwa itumike kuwawezesha wadau kuwafikia wananchi ili kutoa elimu ya afya kwa umma na chanjo ya Uviko 19.

Akitoa salamu kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojioa msemaji wa wizara hiyo Prisca Ulomi amesema wizara hiyo itashirikiana vizuri na wadau na makampuni ya simu kutoa elimu ya afya kwa umma kwa njia ya Tehama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments