TUME YA UTUMISHI WA UMMA YAPOKEA KERO NA MALALAMIKO YA KIUTUMISHI - KISARAWE


Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji (kulia) akisoma nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa umma na wadau kuhusu kero na malalamiko ya kiutumishi, baada ya kuwatembelea Maafisa wa Tume waliokuwa wakipokea changamoto za kiutendaji za watumishi Wilaya ya Kisarawe, Pwani wakati huu wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma pamoja nae ni Maafisa wa Tume Bw. Robert Lwanji (kushoto) na Bibi Florence Kazuva (Picha na PSC).
Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Umma (kutoka kushoto) Bw. Robert Lwanji, Bw. Lamech Mapunda na Bw. Justine Jackson wakisoma vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa na mdau wa Tume (kulia). Maafisa wa Tume walikuwa Wilaya ya Kisarawe, Pwani kishughulikia kero na malalamiko kutoka kwa watumishi wa umma, katika Kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma, mwaka 2021. 


KATIBU wa Tume ya Utumishi wa Umma Bwana Nyakimura Muhoji (aliyevaa shati katikati) katika picha ya pamoja na Maafisa wa Tume walioshiriki katika kupokea na kusikiliza kero, malalamiko na changamoto za kiutendaji kutoka kwa watumishi wa umma na wadau Wilaya ya Kisarawe-Pwani tarehe 16-18 Juni 2021 katika kuadhimisha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2021. (picha na PSC).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments