MHUBIRI MAARUFU TB JOSHUA AFARIKI DUNIA


Mhubiri wa kimataifa, Temitope Balogun Joshua maarufu TB Joshua amefariki dunia.

TB Joshua ni mwanzilishi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (Scoan) na kituo cha televisheni cha Emmanuel TV ambacho amekuwa akikitumia katika mahubiri yake na kuwavutia watu wa mataifa mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa na kanisa lake la Scoan iliyotolewa leo alfajiri inaeleza kwamba TB Joshua alifariki jana Jumamosi Juni 5, 2021 nchini Nigeria muda mfupi baada ya kutoa huduma katika kanisa hilo Jumamosi.

Taarifa hiyo ilisema: Mungu amechukua maisha ya mhudumu wake TB Joshua kulingana na uwezo wake. Amefariki akimuhudumia Mungu.

Taarifa hiyo imetaja sura moja katika biblia inayosema : Mungu muweza hawezi kufanya lolote bila kutoa mipango yake kwa watume wako. " - Amos 3: 7

"Mungu amemuita nyumbani Nabii TB Joshua kwa mapenzi yake. Nyakati zake za mwisho hapa duniani alizitumia katika huduma ya Mungu. Hiki ndio kitu alichozaliwa kukifanya, alikiishi na kukifia," inaeleza taarifa hiyo.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaeleza chanzo cha kifo chake huku ikiwataka waumini kumwombea mhubiri huyo na kuwapa nafasi wanafamilia kuomboleza kifo cha mpendwa wao.

Siku ya Jumamosi tarahe 5 Juni 2021, mtume TB Joshua alizungumza katika mkutano wa runinga ya Emmanuel.
alisema 'kila jambo na wakati wake, kuna wakati wa kuja hapa kwa maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya ibada'."

TB Joshua alikuwa mmoja ya wahubiri maarufu ambapo alijulikana kwa kutabiri matukio yajayo ambayo wengi waliona kama uingiliaji kazi ya Mungu.

Mwaka 2014, Muhubiri huyo alikosolewa nchini Nigeria baada ya upande mmoja wa paa la kanisa lake nchini humo kuanguka na kuwaua takriban watu 116.

Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.

TB Joshua anajulikana kuwa muhubiri Mkristo anayehubiri katika runinga.

Ndiye mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambalo uhubiri moja kwa moja katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos,nchini Nigeria.

TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Marekani ya kusini.

Mwaka 2015 wakati wa mbio za uchaguzi mkuu zikiwa zimepamba moto nchini Tanzania, TB Joshua alikwenda nchini Tanzania na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na mgombea wa CCM, Hayati Dr. John Pombe Magufuli.


Chanzo - MITANDAO YA KIJAMII

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments