CHELSEA YATWAA TAJI LA MABINGWA ULAYA, YAICHAPA MAN CITY 1-0 URENO | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, May 30, 2021

CHELSEA YATWAA TAJI LA MABINGWA ULAYA, YAICHAPA MAN CITY 1-0 URENO

  Malunde       Sunday, May 30, 2021

TIMU ya Chelsea imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester City usiku huu Uwanja wa Do Drag√£o Jijini Porto, Ureno.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 42 akimalizia pasi ya kiungo mwingine wa kimataifa wa England, Mason Mount.

Hilo linakuwa taji la pili tu la Ligi ya Mabingwa kwa The Blues baada ya lile walilolitwaa msimu wa 2011–2012 wakiwafunga wenyeji, Bayern Munich katika fainali Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 chini ya kocha wa muda, Mtaliano Roberto Di Matteo.

Ushindi huu ni mwendelezo wa ubabe wa kocha Mjerumani, Thomas Tuchel kwa kocha Mspaniola wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Pep Guardiola baada ya kuifunga pia Man City 1-0 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA Aprili 17 na 2-1 kwenye ligi Mei 8.

 Via Binzubeiry blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post