RAIS SAMIA AMTEUA AZZA HILAL HAMAD KUWA KATIBU TAWALA WA MKOA WA SIMIYU


Azza Hilal Hamad
***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala Mikoa. Miongoni mwa walioteuliwa ni aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Lakini pia aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga , Albert Msovela amehamishiwa mkoa wa Mara huku  Balozi Batilda Salha Buriani akiteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Balozi Batilda amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Japan


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post