DPP AWAFUTIA MASHTAKA VIGOGO WA MSD | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, May 13, 2021

DPP AWAFUTIA MASHTAKA VIGOGO WA MSD

  Malunde       Thursday, May 13, 2021

 

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistiki Byekwaso Tabura leo Mei 13, 2021 wameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kutokuonesha nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.

Wameachiwa chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20 iliyofanyiwa maitio mwaka 2019. Ambacho kinampa mamlaka DPP kuondoa kesi mahakamani wakati wowote

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele baada ya wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon kuwasilisha mahakamani hapo hati ya kuwafutia mashtaka (Nolle Prosequi) washtakiwa iliyosainiwa na aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga Mei 10,2021 akionesha kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo utakatishaji fedha haramu zaidi ya Sh bilioni 1.6.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 maeneo mbalimbali ya jiji na mkoa wa Dar wa Salaam wakiwa watumishi wa umma kwa pamoja walitengeneza genge la uhalifu kwa ajili ya kujipatia faida.

Pia washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia MSD hasara ya Sh 3,816,727,112.75.

Inadaiwa Bwanakunu akiwa ni mtumishi wa umma alifanya matumizi mabaya ya madaraka kwa kongeza mishahara na posho za wafanyakazi bila ruhusa ya Katibu Mkuu Utumishi na kuisababishia MSD hasara ya Sh Sh 85,199,879.65.

Pia ilidaiwa kati ya Julai 1, 2016 na June 30, 2019 katika maeneo ya tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania washtakiwa hao kwa pamoja waliruhusu uhifadhi mbaya wa vifaa tiba uliosababisha vifaa hivyo kuharibika na kuisababishia MSD hasara ya Sh 85,199,879.65

Katika shtaka la mwisho ilidaiwa kati ya Julai 1, 2016 na June 30, 2019 katika maeneo ya Keko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar wa Salaam wote kwa pamoja walijipatia fedha Sh 1,603,991,095.37 wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu ambao ni kuongoza genge la uhalifu
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post