Maajabu ya Dunia : HII NDIYO MIMEA 7 INAYOKULA NYAMA NA WADUDU | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, May 1, 2021

Maajabu ya Dunia : HII NDIYO MIMEA 7 INAYOKULA NYAMA NA WADUDU

  Malunde       Saturday, May 1, 2021
Mimea mingine hukua mahali ambapo haiwezi kupata virutubisho vyote vinavyohitaji kutoka kwenye mchanga. Ili kuhakikishi mimea hii inapata madini hayo bila kupungua, mimia hiyo hutega, kukamata na kisha kuwala wadudu. Mtego wa kukamata nzi wa Venus (Venus-flytrap) ni mmea ulio na majani yaliyoumbwa mfano wa mdomo ambao hufunga wakati nzi wanapotua hapo. Majani ya mmea wenye umbo la mtungi (pitcher plant) nayo ni mtego wenye utelezi ambao una majimaji ya kumeng'enya ndani. Wadudu na wanyama wanapoanguka humo humeng'enywa.

1. Venus Mtego wa nzi (Venus Flytrap)
Mtego huu wa nzi ni moja ya mimea (jina la spishi Dionaea muscipula) inayojulikana zaidi ambayo hula nyama na hula zaidi wadudu na wale wenye miguu minane (arachnids). Mmea mdogo ulio na majani karibu manne hadi saba ambayo hukua kutoka kwenye shina fupi, na kufanya mitego. Kulingana na Listverse, mmea huo ni wa kushangaza sana kwani unaweza kutambua tofauti kati ya hai na kilichokufa na majani hayo yenye mitego huweza kufunga kwa sekunde 0.1. Ingawa kuna aina moja tu ya spishi ya Venus Flytrap, kuna aina nyingi.

2. Midumu-mwitu (Monkey cups)
Hupatikana katika maeneo ya tropiki mfano Borneo, Sumatra na Malaysia. Mmea huu (jina la spishi Nepenthes) unaokula nyama unaitwa hivyo kwa kuwa nyani wameonekana wakinywa maji yanayojikusanya kwenye vikombe vyake kwenye maeneo ya mvua nyingi misituni, kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Hungry Plants, majani ya mmea huu ambayo huwa mfano wa jagi la maji (pitcher) huweza kuhifadhi maji kiasi cha zaidi ya lita. Vikombe hivyo hukusanya maji ambayo hutumia kumeng'enya wadudu.

3. Umande wa jua (Sundew)
Kuna karibu spishi 200 za Sundew, na zote hutofautiana sana kwa sura, saizi na mahitaji ya kukua. Nyingi ya spishi hizo (Drosera) zimefunikwa kwenye nyuzi ambazo zina ncha zenye gundi, na ripoti ya Carnivorous Plants UK inasema kwamba nyuzi hizi zinaweza kusonga, na kusaidia kwa haraka kukamata, kunyonga na kutafuna wadudu ambao watakuwa wamekamawama.

4. Butterworts
Butterworts, au mitego ya karatasi yenye dutu za kunata zilizo na sumu unaweza kuwa hai au ya kuwa kimya na kutegemea kamasi inayonata kwenye jani kukamata mawindo. Spishi hii ya Pinguicula ambayo ipo katika orodha ya maua yanayodondoka rahisi (orchid), pia hujulikana kwa maua yake ya kupendeza kwa rangi ya manjano, nyekundu, zambarau au nyeupe. Mimea hii ya kumeng'enya hupenda kula mbu na kawaida hupatikana huko Marekani.

5. Vifuko vya kunyonya (Bladderworts)
Jina hili linatokana na vifuko vidogo vinavyopatikana kwenye mmea huu (jina la spishi genus Utricularia) na ni aina ya mmea katika jamii ya inayokula nyama na hupatikana kwenye maji wazi na hunasa wadudu kwenye kifuko mfano wa balbu inayonyonya. Kulingana na Botanical Society of America, nywele ndogo za kugusa mlangoni pa kifuko hujua wakati wadudu, mfano nzi, wanapotua kwenye mmea huo, ambao husababisha kifuko kilichosinyaa au kulegea kutanuka mara moja, kikanyonya maji, na kumfungia kisha kumla mnyama huyo.

6. Mimea yenye mtungi wa kunasia kamba (Lobster-pot plants)

Jina hili linatokana na mtungi uliotumiwa na wavuvi kunasia samaki aina ya kamba (lobsters), mmea huu (Jina la spishi ni Darlingtonia californica) hula nyama na hunasa mawindo yake yanapoingia kwenye mtego wake, ambao unafanana na mtungi wa kunasia kamba. Windo hushindwa kufahamu njia ya kujinasua, na nywele kwenye mtego huo hujikunja na kulazimisha windo kwenda chini ya jani ambapo humeng'enywa.

7. Mtengo wa manati ya kunasa nzi (Catapulting flypaper trap)
Aina hii ya mimea ambayo hula nyama ina sifa zote mbili za (kama vile Butterworts) na kunasa (kama Venus mtego wa nzi). Kuenea kwake zaidi ni Australia, mmea huu (Jina la spishi ni Drosera glanduligera) wa kula nyama hunasa mawindo yake kwa kutumia nyuzi zake za nje zenye kunata. Wakati mawindo yanapoweka shinikizo kwenye vishina hivi, chembe za chini za mmea huachia na kufanya windo lililonaswa kuelekea katikati ya mmea, ambapo huliwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post