SIMBA SC YAIKANDAMIZA MTIBWA SUGAR 5G


Mabingwa watetezi, Simba SC wamerejea na moto wao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara na leo wameichapa Mtibwa Sugar 5-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na nyota wa kigeni watupu, Wazambia Clatous Chama dakika ya tisa, Rally Bwalya dakika ya 19, Mnyarwanda Meddie Kagere dakika ya 43 na 52 na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 69.

Ushindi huo unaifanya Simba SC inayofundishwa na Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa ifikishe pointi 49 baada ya kucheza mechi 21 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments