RAIS SAMIA KUKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akilihutubia Bunge la 12 na kuelezea Muelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita leo tarehe 22 Aprili, 2021 Jijini Dodoma
***

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Aprili 22,2021 amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekua Rais Dk John Magufuli ambapo ameahidi kulinda Demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Rais Samia amesema katika kulinda huko Demokrasia amepanga kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kuona namna iliyo bora ya kufanya shughuli zao za kisiasa huku pia akiwataka watanzania kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria za nchi.

"Ili kulinda uhuru wa demokrasia nakusudia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa Tanzania ili kwa pamoja tuweke mwelekeo wa kuendesha shughuli za siasa zenye tija na maslahi ya nchi yetu," amesema.

Amesema katika hilo pia ameiomba Mahakama kupitia Jaji Mkuu kuhukumu yaliyo ya haki kwa wananchi na siyo kutoa hukumu zisizo kuwa na haki na zenye kuwaumiza Wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments