Picha : RAS SHINYANGA, DC MBONEKO WAUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA FLAVIANA KIFIZI

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko wameungana na mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi (40) aliyefariki dunia Aprili 20,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam akiumwa kichwa.

Akizungumza wakati akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 nyumbani kwa Lubaga Mjini Shinyanga, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema Flaviana alijituma na kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha wananchi wa Shinyanga wanapata huduma ya maji safi na salama.

“Taarifa za kifo cha Flaviana zimetushtua sana kama mkoa. Niwaambie tu kuwa hakuna kazi ngumu kama kuwa kiongozi wa taasisi inayohusika kwa sababu maji hayana mbadala. Flaviana alitamani kila eneo, kila uchochoro wa Shinyanga upate huduma ya maji. Tumefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha wananchi wa Shinyanga wanapata maji”,amesema Msovela ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa SHUWASA.

“Flaviana alikuwa msimamizi mzuri na kiungo mzuri katika mkoa wa Shinyanga. Alikuwa msikivu na alipenda kuwa na maamuzi ya pamoja na ndiyo maana SHUWASA imekuwa ikifanya vizuri na imeendelea kukua. Naomba tuenzi mambo aliyoyasimamia na kuyaanzisha na alitamani yafanyike”,ameongeza Msovela.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amesema Flaviana hakubagua watu na alikuwa rafiki wa kila mtu na alitimiza wajibu wake kikamilifu na kuipa sifa nzuri SHUWASA kwa kujali wananchi.

“Kifo cha Flaviana ni pigo kwetu serikali na wananchi kwa ujumla. Flaviana alishirikiana na viongozi wa serikali na wadau katika kuwapatia huduma ya maji wananchi. Hata kama kazi ilikuwa ngumu ukimuagiza kufanya yeye alifanya. Mama yake na Flaviana ni Jasinta na mimi naitwa Jasinta, alikuwa ananiita mama. Naomba tumuenzi kwa mazuri aliyofanya”,amesema Mboneko.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Bi. Mwamvua Jilumbi amemwelezea Flaviana kuwa alikuwa kiongozi Jembe aliyefanikiwa kujenga misingi imara SHUWASA hivyo watamkumbuka kutokana na usikivu,utendaji kazi na bidii yake katika kazi.

“Flaviana alipenda sana kazi yake. Hakuwa Mhandisi lakini alikuwa anafanya kazi kama amesomea uhandisi. Ameitumikia SHUWASA kwa zaidi ya miaka 10 mwanzo akiwa Meneja wa Rasilimali na utawala kisha Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA”,ameongeza Jilumbi.

Mazishi ya mwili wa marehemu Flaviana Kifizi yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Aprili 23,2021 jijini Mwanza.

Marehemu Flaviana Kifizi alizaliwa mwaka 1981, ameacha mtoto mmoja wa kike.

ANGALIA PICHA HAPA
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akitoa salamu za rambirambi wakati akiongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Flaviana Kifizi
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akitoa salamu za rambirambi wakati akiongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akitoa salamu za rambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Mwamvua Jilumbi akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Parokia ya Lubaga, Philemon Chikala akiongoza Ibada ya Kumuombea mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Mwamvua Jilumbi (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akimfariji  (Precious) ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Afisa Habari wa KASHWASA, Dkt. Mwidima Peter akitoa mwongozo wa kuaga mwili wa marehemu Flaviana Kifizi
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akifuta machozi wakati akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Waombolezaji wakiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 

Kushoto ni Mkurugenzi wa KASHWASA, Mhandisi Joshua Mgeyekwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakiwa msibani

ZIFUATAZO NI PICHA ZA WADAU MBALIMBALI WAKITOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za maji nchini akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa RUWASA mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Kayovela akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga. Luther Mneney akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Mwakilishi wa Benki ya NMB akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Afisa Habari wa KASHWASA, Dkt. Mwidima Peter akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Mwakilishi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Sam Bahari akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa KUWASA, akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (Patrobas Katambi), Samwel Jackson akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Diwani wa kata ya Lubaga akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments