NEC YAFANYA MABADILIKO UCHAGUZI MDOGO MUHAMBWE NA BUHIGWE | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, April 10, 2021

NEC YAFANYA MABADILIKO UCHAGUZI MDOGO MUHAMBWE NA BUHIGWE

  Malunde       Saturday, April 10, 2021

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanya mabadiliko ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika majimbo ya Muhambwe na Buhigwe mkoani Kigoma pamoja na kata 18 Tanzania Bara, ambao sasa utafanyika tarehe 16 mwezi Mei mwaka huu badala ya tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu.


 
Akitangaza ratiba ya mabadiliko ya uchaguzi huo, Mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC, – Dkt Wilson Mahera amesema kuwa kufuatia mabadiliko hayo, tarehe ya kuanza kuchukua fomu katika jimbo la Buhigwe ni 24 hadi 30 mwezi huu  na kampeni zitaanza  tarehe moja hadi 15 mwezi Mei.
 
Dkt. Mahera amesema kuwa, mabadiliko hayo yamefanyika ili uchaguzi katika majimbo ya Buhigwe, Muhambwe na kata 18 kumi ufanyike siku moja.

Jimbo la Buhigwe liko wazi  kufuatia aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Dkt. Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na lile la Muhambwe liko wazi kufuatia kifo cha Mhandisi Atashasta Nditiye.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post