WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AWAASA WAKUU WA TAASISI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA


Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb)  amewataka Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu  zinazotumika kusimamia taasisi hizo na sikuwa kikwazo katika kutoa huduma  bora kwa wananchi.

Waziri  Mkumbo  aliyasema hayo alipokuwa akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika kikao na Wakuu wa Taasisi hizo  kilichofanyika  tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini  Dodoma.

“Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Viwanda zinamchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hivyo nawasihi muendelee kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria Kanuni na taratibu zinazosimamia taasisi zenu katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi na si kuwa kikwazo”

Aidha, Wakuu wa Taasisi waliohudhuria kikao hicho kutoka TBS, WMA, BRELA, TANTRADE, SIDO, NDC, EPZA, FCC, FCT, WRRB, TIRDO, CAMARTEC, TEMDO na CBE walipata fursa ya kutoa maoni na changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa Mhe.Waziri wa Viwanda na Biashara.

Waziri Mkumbo ameahidi kuendelea kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka katika taasisi hizo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo upatikanaji Bodi zinazofanya kazi katika kila taasisi ili kurahisisha utoaji wa maamuzi sahihi na kwa wakati.

Naye Naibu Waziri akiongea na Wakuu wa Taasisi hizo, alisema kuwa mchango wa taasisi hizo  ni muhimu na zinategemewa katika kuifanikisha Wizara  kufikia malengo ya taifa katika ukuaji wa viwanda na biashara shindani na hivyo kukuza uchumi wa nchi 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments