MAFURIKO YAUA ZAIDI YA WATU 75 NCHINI INDONESIA NA TIMOR MASHARIKI | MALUNDE 1 BLOG

Monday, April 5, 2021

MAFURIKO YAUA ZAIDI YA WATU 75 NCHINI INDONESIA NA TIMOR MASHARIKI

  Malunde       Monday, April 5, 2021


Zaidi ya watu 75 wamefariki dunia na wengine wengi wahawajulikani waliko baada ya mafuriko na maporomoko ya ardhi kuyakumba baadhi ya maeneo nchini Indonesia na Timor Mashariki, maafisa wa eneo hilo wameisema leo Jumatatu.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa yamesababisha maafa katika maeneo kati ya Flores, chini Indonesia na Timor ya Mashariki, na kusababisha maelfu ya watu kukimbilia katika vituo vya mapokezi.

Mvua hiyo imesababisha mabwawa kujaa maji na kusababisha mafuriko katika maeneo ambapo maelfu ya nyumba zimeharibika, wakati waokoaji wamekuwa wakijitahidi kutoa msaada kwa waathiriwa.

"Kuna watu 55 wamefariki dunia, lakini idadi hii inaendelea kubadilika, kwani watu 42 bado hawajulikani waliko," amesema Raditya Djati, msemaji wa Idara ya majanga na usaidizi wa kibinadamu nchini Indonesia kwenye televisheni ya MetroTV.

Takriban watu 21 wameuawa katika Timor Mashariki, kulingana na afisa wa Timor. Vifo vingi vilitokea katika mji mkuu wa Dili.

Mashariki mwa kisiwa cha Flores cha Indonesia, nyumba nyingi, barabara na madaraja vilifunikwa na matope, na kufanya hali kuwa ngumu kwa waokoaji kujaribu kufikia maeneo yaliyoathiriwa zaidi.

Credit:RFIUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post