RAIS SAMIA AAGIZA VYOMBO VYA HABARI VILIVYOFUNGIWA TANZANIA VIFUNGULIWE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, April 6, 2021

RAIS SAMIA AAGIZA VYOMBO VYA HABARI VILIVYOFUNGIWA TANZANIA VIFUNGULIWE

  Malunde       Tuesday, April 6, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
**
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kufunguliwa mara moja kwa kwa vyombo vya habari vilivyofungwa na Wizara inayohusika ihakikishe vyombo vya habari vinafuata sheria na miongozo iliyowekwa.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumanne Aprili 6,2021 wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu wa taasisi na Idara mbalimbali Ikulu Jijini Dar es salaam.

Amesema siyo vyema kutumia mabavu (nguvu) katika kuchukua hatua za kufunga vyombo vya habari na kuagiza wahusika kutotumia ubabe kuvidhibiti.

"Nasikia kuna Vi Tv vya mkononi ,vyombo vya habari mlivifungia, vifungulieni na vifuate sheria, tusiwape mdomo kwamba tunaminya uhuru wa kuzungumza. Tusifungie kibabe, wafungulieni na kuhakikisha wanafuata kanuni na miongozo ya Serikali",amesema Rais Samia.

"Watakapofanya makosa adhabu zitolewe kulingana na sheria inavyoelekeza, viacheni vifanye kazi yao isionekane wanazuiwa kuongea", amesema Samia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post