MKE ADAI TALAKA KISA MME KASHINDWA KUFANYA NAYE TENDO LA NDOA MIAKA 5 | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, April 6, 2021

MKE ADAI TALAKA KISA MME KASHINDWA KUFANYA NAYE TENDO LA NDOA MIAKA 5

  Malunde       Tuesday, April 6, 2021


Adela Ngogolo (42) amefungua kesi ya madai mahakama ya mwanzo Ilala akiomba kupewa talaka na mumewe, Alcado Mkondola (62) kwa madai kuwa ameshindwa kumpatiwa haki yake ya tendo la ndoa kwa miaka mitano mfululizo.

Mwanamke huyo anayeishi na mumewe Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam ameieleza mahakama hiyo leo Jumanne Aprili 6, 2021 kuwa Mkondola hataki kushiriki tendo la ndoa kwa muda wa miaka mitano na kila akijaribu kumuomba unyumba anasukumwa na kuambiwa akalale chumba cha watoto.

Kesi hiyo ya madai namba 6/2021 aliifunguliwa mahakamani hapo Februari 25, 2021 na inasikilizwa hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Benjamin Mwakasonda.

Mwanamke huyo amedai mahakamani hapo kuwa kutoshiriki tendo hilo kwa muda mrefu kumesababisha apate madhara mbalimbali ikiwemo kuugua fangasi sehemu za siri kutokana na kujiingizia vitu visivyofaa ili kutuliza hamu.
Chanzo - Mwananchi

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post