RAIS SAMIA : UKIZINGUA TUTAZINGUANA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza watendaji wa serikali kujituma kufanya kazi akisisitiza kuwa atazinguana na watakaozingua.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 6,2021 wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu wa taasisi na Idara mbalimbali Ikulu Jijini Dar es salaam.

“Wewe ni kijana mimi ni mama ukinizingua tutazinguana,” ni kauli ambayo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (Tasac), Kaimu Mkeyenge baada ya kula kiapo cha uaminifu.

Katika maelezo ya Rais amesema amemteua Mkeyenge kushika nafasi hiyo ili asafishe madudu yaliyopo kwenye taasisi hiyo.

“Ulikuwa ndani ya Tasac unayajua madudu yaliyopo. Jambo lililoniudhi zaidi kwa mwaka mmoja mmefanya vikao 23 vya bodi na imetumiwa karibu Sh600 milioni, ukiangalia kilichozungumzwa na tija ya vikao hivyo hakuna.”

“Nataka ukafanye kazi na sio kwenda kupandisha mabega kwa wenzio uliowaacha, kama kuna makundi ukayaondoe, tunataka Tasac izalishe. Nasisitiza kafanye kazi ukinizingua tutazinguana,” amesema Rais Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments