MCHEZAJI WA SOKA SOSPETER MAIGA AFARIKI DUNIA AKIFANYA MAZOEZI MUSOMA MJINI


Mchezaji wa zamani wa klabu ya Biashara United Mara, Sospeter Maiga Mandala amefariki dunia asubuhi ya leo wakati akifanya mazoezi katika uwanja wa Posta mjini Musoma.

Kwa mujibu wa wachezaji waliokuwa mazoezini na mchezaji huyo, Mandala alifika mazoezini kama kawaida akiendesha baiskeli yake na kufanya mazoezi vizuri bila kuonyesha dalali zozote lakini ghafla aliinama na kushika kifua.

"Tumeanza mazoezi vizuri asubuhi na leo alikuwa anakimbia sana na kutoa pasi, lakini ghafla aliinama na kushika kifua, tulipokimbia kumuona akaonekana amepoteza fahamu, lakini tulipomfikisha hospitali ikaonekana amefariki dunia," alisema mchezaji huyo.

"Hata hivyo, hadi. sasa bado hatujapata taarifa za daktari aliyempokea ili kubaini nini kimesababisha kifo chake,".

Mchezaji huyo inaelezwa hii ilikuwa Mara ya tatu kuanguka lakini wakati wote hakuwa wazi ili kupata matibabu ya tatizo la moyo linalosemekana lilikuwa linamsumbua, “ alisema mmoja wa wachezaji aliokuwa nao mazoezini kabla ya kifo chake.

Mbali na Biashara, marehemu Mandala pia amewahi kuchezea timu za Nyakato FC, Kigera FC, JK FC, Pamba FC za Mwanza, Geita FC ya Geita, Stand United ya Shinyanga na Njombe Mji FC ya Njombe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments