MSANII WA HIPHOP NA MUIGIZAJI DMX AFARIKI DUNIA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, April 9, 2021

MSANII WA HIPHOP NA MUIGIZAJI DMX AFARIKI DUNIA

  Malunde       Friday, April 9, 2021Picha ya DMX enzi za uhai wake

Taarifa na vyanzo mbalimbali vya habari nchini Marekani vimeripoti kuhusu kifo cha msanii wa HipHop na Muigizaji Earl Simmons maarufu kama DMX ambaye hadi umauti unamkuta alikuwa na umri wa miaka 50.

DMX amefariki dunia siku ya leo Ijumaa April 9 katika Hospitali ya White Plains Hospital iliyopo Jijini New York, Marekani.

Chanzo cha kifo chake inasemekana kuwa ni kuzidisha matumizi ya madawa za kulevya na kupata mshtuko wa moyo, wiki iliyopita iliripotiwa kuwa alikimbizwa Hospitali kutokana na tatizo hilo.

Kwenye muziki msanii huyo alitamba na nyimbo kadhaa kama Get at me dog, Ruff ryders anthem, Money power respect, party up na kwenye upande wa kuigiza alicheza filamu kama Cradle 2 the grave, Belly, Never Die Alone, Beef, Beyond the law na nyinginezo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post