Kila Mwananchi Kupata Nafasi Ya Kuuaga Mwili ya Hayati Dr Magufuli- Chato | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, March 25, 2021

Kila Mwananchi Kupata Nafasi Ya Kuuaga Mwili ya Hayati Dr Magufuli- Chato

  Malunde       Thursday, March 25, 2021


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema kuwa kila mwananchi aliyefika katika Uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita atapata nafasi ya kupita pembeni ya jeneza lenye mwili wa wa Dkt. John Magufuli kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Amewataka Wananchi kuwa watulivu, kwani hata kama itafika usiku, lakini lazima kila mmoja atapata nafasi ya kuaga.

Ameeleza kuwa, utaratibu uliotumika katika baadhi ya maeneo wa kuzungusha mwili uwanjani mwili wa Dkt Magufuli hautatumika wilayani Chato, na ndiyo sababu walitenga siku moja kwa ajili ya wakazi wa Geita na maeneo jirani.

Akizungumza kuhusu msiba huo, Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema haujaigusa Tanzania pekee bali hata nchi za mbali na Jumuiya ya Kimataifa kutokana na utendaji kazi wa Dkt Magufuli ambao uliwaridhisha wengi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post