WAZIRI MKUU : MAMA MZAZI WA HAYATI MAGUFULI BADO NI MGONJWA, YUPO KITANDANI MIAKA MIWILI SASA


Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Joseph Magufuli (kulia,) akiwa na mama yake mzazi Suzana Magufuli ambaye ni mgonjwa hadi sasa na Serikali imeahidi kusimamia matibabu yake hadi atakaporejea katika hali yake ya kawaida.
***

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema mama mzazi wa Hayati Rais Dkt.John Joseph Magufuli bado ni mgonjwa na yupo kitandani kwa miaka miwili sasa na Serikali itahakikisha madaktari wanamtibu hadi atakaporejea katika hali yake ya kawaida.

Akizungumza leo Wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati JPM, Majaliwa amesema hadi sasa mama mzazi wa Hayati Rais Magufuli yupo kitandani akiendelea na matibabu.

"Nimeongea na Mh. Rais kuhusiana na jambo hili na tutahakikisha madaktari wanamtibu bibi yetu hadi pale atakaporejea katika hali yake ya kawaida." Amesema Majaliwa.

Waziri Majaliwa msiba huo umewagusa watanzania wengi na kama Taifa hawana budi kumshukuru Mungu na kumuenzi Hayati JPM kwa vitendo.

Pia amewashukuru wasanii, waandishi wa habari na watanzania kwa ushirikiano wanaoonesha katika kipindi chote cha maombolezo.
 
Chanzo - Michuzi blog

UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments