KAMPUNI YA MACLEANS YAOMBOLEZA KIFO CHA HAYATI MAGUFULI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, March 26, 2021

KAMPUNI YA MACLEANS YAOMBOLEZA KIFO CHA HAYATI MAGUFULI

  Malunde       Friday, March 26, 2021


Dkt. John Pombe Magufuli

Kampuni ya Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ,Malaika Cleaning Service (Macleans) ya jijini Dar es salaam imeungana na Watanzania kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Macleans , Alloysius Madata amesema Kampuni yake imepokea kwa masikitiko makubwa sana msiba huu wa kitaifa wa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John  Magufuli kwani alikuwa chachu thabiti ya maendeleo endelevu ya taifa la Tanzania.

Madata amesema Dkt. Magufuli, alikuwa mtetezi wa wanyonge na alionyesha kuwajali na kuwapenda na ndiyo chanzo cha wajasiriamali wengi kuinuka kiuchumi na maisha yao ya kila siku.

Aidha amesema kampuni yake itaendelea kumuenzi na kuyaenzi mambo yote muhimu ikiwa pamoja na maendeleo aliyotuletea katika taifa

Amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushika usukani wa kuliongoza Taifa na kwamba anamuombea kwa Mungu aweze kutekeleza vyema majukumu yake.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE,AAMEN!!
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post