MAREKANI YATISHIA KUIWEKEA VIKWAZO NCHI MYANMAR | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, February 2, 2021

MAREKANI YATISHIA KUIWEKEA VIKWAZO NCHI MYANMAR

  Malunde       Tuesday, February 2, 2021


 Rais wa Marekani Joe Biden ametishia kuirejeshea Myanmar vikwazo baada ya jeshi kupindua serikali.

Jeshi la Myanmar lilimkamata Aung San Suu Kyi na viongozi wengine wa kisiasa wakiwashutumu kwa udanganyifu katika uchaguzi wa hivi karibuni ambao Suu Kyi alipata ushindi mkubwa.

Katika taarifa, Biden amesema "nguvu isiwahi kutumika kubadilisha maamuzi ya watu au kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika kwa njia ya halali".

Umoja wa Mataifa na Uingereza pia zimeshutumu mapinduzi hayo.

Marekani ilikuwa imeiondolea nchi hiyo vikwazo zaidi ya muongo mmoja uliopita wakati ambapo Myanmar ilionesha kufuata demokrasia.
 

Biden amesema hatua hiyo itapitiwa tena kwa haraka na kuongeza: "Marekani itaunga mkono demokrasia kila itakapokuwa hatarini."Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post