WANAUME WATAKIWA KUVUNJA UKIMYA KUHUSU UKATILI WANAOFANYIWA
Tuesday, February 02, 2021
Na Mwandihsi Wetu Dodoma
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wanaume kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kuhusu ukatili wanaofanyiwa ili kutokomeza matukio ya ukatili nchini.
Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipotoa tamko kuhusu Vitendo vya Ukatili katika jamii mbele ya waandishi wa habari.
Gwajima amesema vitendo vya ukatili vimezidi kuongezeka hapa nchini akitolea mifano mbalimbali iliyotokea hivi karibuni ya waanfamilia kufanyiana vitendo vya kikatili.
Amesema ukatili haufanywi kwa wanawake na watoto tu lakini hata kwa makundi mengine ikiwemo wanaume lakini wengi wao wamekuwa wakikaa kimya.
"Wanaume msione aibu, muache kukaa kimya dhidi ya vitendo vya ukatili mnavyofanyiwa. Toeni taarifa mapema kwa mamlaka husika muweze kupata msaada ili kuzuia madhara zaidi kutokea" amesema Gwajima.
Amezitaja sababu za ukatili huu ni pamoja na migogoro ya kifamilia ikiwemo kugombea mali, matatizo ya kisaikolojia na jamii kutotekeleza wajibu wake wa kutunza na kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya familia.
Dkt Gwajima amesema Wizara itaendelea kuchukua jitihada zote kuhakikisha ukatili unatokomezwa kwa makundi yote, lakini jamii pia ina jukumu la kuwalinda makundi yote.
Aidha, amesema Wizara itaendelea kushughulikia mauaji ya wazee na kuwa haitorudi nyuma kupambana na ukatili wa aina yoyote ili nchi na mipaka yake ibaki salama kwa amani, upendo na kujiletea maendeleo.
Naye Afisa Ustawi Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Amina Mafita amesema Wizara imejikita zaidi katika kuelimisha jamii kwa kuunda mabaraza kuanzia ngazi za vijiji na mitaa kwa lengo la kulinda makundi yote.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin